RIPOTI: Snapchat Kuununua Mtandao Wa Vurb!

0
Sambaza

Wengi wanaweza wakawa hawaijui App ya vurp, lakini kwa haraka haraka huduma hiyo inawawezesha watu kugundua ni vitu gani viko karibu nao.

Kwa mfano unaweza ukagundua migahawa, picha za sinema au vitu vingine vingi. Vurb ilianzishwa mwaka 2011 (kama TeknoKona vile) na pia ikaanzishwa kama App katika vifaa vya iOS mwaka 2015 na baadae iliweza kutanua mabawa kwa vifaa vya Android na Amazon.


Snapchat inasemekana kuwa inanunua huduma hiyo kwa jumla ya takribani dola 110 za kimarekani.

SOMA PIA:  Mwizi wa simu 100 na zaidi akamatwa kisa app ya Find My iPhone

Uzuri wa Vurb ni kwamba ukishaona kile unachokitafuta karibu yako kwa mfano mgahawa, App itatoa taarifa za muhimu kuhusiana na kitu hicho kama vile uchambuzi, maelekezo ya jinsi ya kufika. Pia kwa kutumia App hiyo unaweza ukaita gari kwa kutumia huduma ya Uber ili ikupeleke sehemu uliyoiona kwa kutumia Vurb kwa mfano kupelekwa katika mgahawa.

Bado haipo wazi kuwa Vurb baada ya kununuliwa bado itajitegemea au vipengele vyake vitaingizwa katika App ya Snapchat.

SOMA PIA:  SanDisk imeleta memori kadi ya ukubwa wa GB 400

Uongozi wa Snapchat ulipo ulizwa uligoma kutoa tamko lolote juu ya jambo hili.

App Ya Vurb

App Ya Vurb

Snapchat imejipatia umaarufu mkubwa sana tena kwa kipinidi cha muda mchache sana na hii imewafanya mpaka wapinzani wake waanze kuiga baadhi ya vipengele ambavyo vinapatikana katika App ya Snapchat.

Niambie kwa upande wako unahisi nini itakua ndio matunda ya Ununuzi wa huduma hii kwa Snapchat, yaani wataitumiaje? Ningependa kusikia kutoka kwako, niandikie hapo chini sehemu ya comment.

SOMA PIA:  Kufunga/kufungua 'usb ports' za kwenye kompyuta #Maujanja

Ripoti Hii Ni Kwa Mujibu Wa Mtandao Wa The Information

Tembelea TeknoKona kila siku ili kuwa karibu na habari na maujanja mbalimbali yanayohusu teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com