RIPOTI: Twitter Imewekeza $70M Kwenye Mtandao Wa SoundCloud! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

RIPOTI: Twitter Imewekeza $70M Kwenye Mtandao Wa SoundCloud!

0
Sambaza

SoundCloud wamepokea uwekezaji mpya kutoka katika mtandao maarufu wa kijamii, Twitter. Twitter imewekeza dola za kimarekani milioni 70, kutokana na ripoti zinavyosema.

can i buy amoxicillin online uk

go site Kampuni hiyo ya kutoka huko Berlin, baada ya kupokea pesa hiyo inasadikiwa kuwa na hadhi ya takribani dola milioni 700 za kimarekani.

how can i buy Phenytoin Logo Ya SoundCloud

Mpaka sasa kwa haraka haraka mtandao wa SoundCloud unatembelewa na watu milioni 175 kwa mwezi. Mtandao huu ndio ule ambao unatoa huduma ya muziki kutoka kwa wasani na ma DJ wachanga bila kuacha wale ambao ni tayari maarufu


Twitter walipoulizwa walikataa kuchangia kitu kuhusiana na jambo hili. Ukiachana na kutofanya vizuri kwa kampuni ya SoundCloud bado Twitter lengo lao halikufa. Kumbuka kati ya mwaka 2012 na 2013 kampuni ya soundcloud ilipata hasara ya kiasi cha dola milioni 70 za kimarekani

Mwanzoni mwaka huu kampuni iliamua kubadilisha mfumo wake mzima na pia ukafanya maboresho kwa kuanzisha huduma ya muziki wa ku ‘Stream’ kwa malipo kwa kipindi Fulani (Mwisho wa mwezi, mwaka n.k)

Muaonekano Wa App Ya Twitter Na SoundCloud Katika Simu

Muaonekano Wa App Ya Twitter Na SoundCloud Katika Simu

Licha ya SoundCloud kufanyaga vibaya lakini bado wataalamu wa mambo ya teknolojia wanatabiri kuwa bado mtandao huo utazidi kupeta tuu.

Niandikie sehemu ya comment hapo chini, je wewe unaona ni sawa kwa kampuni ya Twitter kwenda na kuwekeza katika kampuni ya SoundCloud? Kumbuka kampuni hiyo huwa haifanyi vizuri sana katika swala zima la kutengeneza faida

Tembelea TeknoKona kila siku kwa habari kadha wa kadha zinazohusu maswala mazima ya teknolojia. Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.