Roboti kupokea wageni hospitalini! #Teknolojia - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Roboti kupokea wageni hospitalini! #Teknolojia

1
Sambaza

Hivi karibuni hospitali  mbili nchini Ubeligiji zimeamua kutumia roboti kufanya kazi ambazo binadamu angeweza kuzifanya.

Roboti wamekuwa wakifanya kazi nyingi na hivyo kupunguza umuhimu wa kuajiri binadamu kwa ajili ya kufanya kazi hizo.

Roboti huyo anayefahamika kwa jina “Pepper”, aliyotengenezwa kuelewa hisia za watu inatarajiwa kuanza kazi mpya kama karani wa mapokezi.

source site Pepper ana urefu wa kina futi nne na ana uwezo wa kutambua sauti za binadamu kwa lugha 20 pia ana uwezo wa kubaini iwapo anazungumza na mwanamume, mwanamke au mtoto. Roboti huyo itakuwa ya kwanza kuhudumu katika jumba la matibabu baada ya roboti nyengine kuwekwa katika maduka mbalimbali, benki na vituo vya treni.

Pepper Roboti kupokea wageni

buy flagyl online us Pepper akifanya kazi ya ukarani hospitalini.

Hospitali moja ina mipango ya kuajiri roboti zaidi kwa miaka 10 ijayo ingawa baadhi ya wataalamu wamehoji umuhimu wa roboti za kijamii kama vile Pepper. Teknolojia ya utumiaji wa robot inazidi kukua siku baada ya siku kwani siku hizi robots wanatumika kufanya upasuaji na hivyo kupunguza uwezekano wa makosa kufanyika wakati wa upasuaji.

Roboti kutumika kama karani wa mapokezi kwa namna moja au nyingine itasababisha ukosefu wa ajira kwa watu wengi ambao kazi zao zinaweza fanywa na roboti. Kwa upande mwingine utumiaji wa roboti utapunguza mabishano kati ya wawili kwani roboti hata kama roboti akikosea anaweza kurekebisha makosa yake kwa haraka sana tofauti na binadamu.

Robot "Nadine" anayefanana kabisa na binadamu

can i buy femara over the counter Robot “Nadine” anayefanana kabisa na binadamu

Kutokana na kwamba roboti huyo kujua lugha takribani 20 hospital hizo zitakuwa zikipata wagonjwa kutoka mataifa mbalimbali kutokana na uwepo wa roboti huyo kwani atakuwa na uwezo wa kuongea na wagonjwa hao hata kama hospitalini hapo hakuna anayeelewa zaidi lugha anayoongea hivyo basi roboti huyo kuwa mkalimani kati ya mgonjwa na muuguzi/daktari.

Kutokana na kwamba roboti huyo anajua lugha 20 hospital haihitaji kuajiri mkalimani kufanya kazi ya kutafasiri kutokana na kazi hiyo inaweza kufanywa na roboti.

[socialpoll id=”2363006″]

Chanzo: BBC, The Telegraph

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|