Roketi ya Space X yatumika kwa zaidi ya safari moja! #Anga

0
Sambaza

Imekuwa kama jambo la kawaida kwa Space X kufanikiwa katika suala zima la urushaji wa roketi kwani hivi karibuni kampuni hiyo inayojishughulisha na masuala ya anga imefanikiwa kurusha roketi bila matatizo yoyote.

Space X iliyo na makao yake huko Carlifonia, Marekani, imefanikiwa kurusha tena roketi yake kwa kutumia moja ya roketi zake aina ya Falcon 9. Awamu ya kwanza ya roketi hiyo ambayo ilitumika tena miezi 11 iliyopita, ilitumiwa kutuma satellite ya mawasilano kuenda kwa mzingo wa dunia, kutoka kituo cha safari za anga za juu cha Kennedy Space Center.

Falcon 9 ikiwa tayari kupaa kutoka kituo cha Kennedy Space Center.

Kitendo cha Space X kuweza kutumia roketi moja kwa safari zaidi ya moja ni hatua kubwa kwa kampuni hiyo iliyoonyesha kuwa haikubahatisha mara ya kwanza ilipoweza kutumia roketi inafahamika kama Falcon 9 na ikarudi salama.

Falcon 9 ilipotumika mara ya kwanza ilirudi na kutua salama baharini.

Kwa miaka miwili iliyopita SpaceX imekuwa ikirudisha sehemu za kwanza za roketi zake ardhini baada ya sehemu hizo kutimiza wajibu wa kuinua mzigo ulitundikwa juu yake. Sehemu hizo za kwanza hurudi peke yao na kutua salama katika chombo kinachoelea baharini. Teknolojia hii inasaidia kupunguza gharama ya safari hizo kwa kiasi kikubwa sana ukilinganisha na zamani.

Sehemu hiyo ya kwanza hupaa kwa takriban dakika mbili kabla ya kuchomoka na kurudi ardhini.

 

SpaceX ina lengo za kuzikarabati na kuzitumia tena roketi ambazo tayari zishatumika kwa minajili ya kupunguza gharama na sasa sehemu zingine za kwanza zilizorudi na kutua salama zitatumiwa tena kurusha roketi zingine mwaka huu.

Vyanzo: BBC, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Elon Musk: Nenda kokote duniani ndani ya lisaa, usafiri kwenda Mirihi (Mars) unakuja
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com