Row-bot: Fahamu Roboti Mdogo Anayesafisha Maji bila Kuitaji Kuchajiwa Kamwe

1
Sambaza

Teknolojia ya utengenezaji roboti wadogo na wakubwa wanaosaidia kazi mbalimbali kufanyika kuanzia viwandani hadi majumbani unazidi kukua. Ila roboti wote huwa wanaitaji kuchajiwa na mara nyingi inakuwa kwa kutumia umeme, leo mfahamu roboti mdogi anaye enda kwa jina la Row-bot asiyeitaji kuchajiwa kamwe.

Kuna watafiti mbalimbali duniani wanaojituma kwa nguvu kubwa kuja na teknolojia na vitu kama roboti ambavyo vinasaidia katika mambo ya kijamii badala ya kutengeneza bidhaa za kibiashara.

Muonekano wa Row-bot

Muonekano wa Row-bot

Kwa kifupi roboti huyu – ‘kupitia bakteria spesheli walio ndani yake’ atakuwa anakula vijidudu vyote vyenye madhara na hivyo kusafisha maji hayo.
Row-bot imetengenezwa kuweza kuelea kwenye maji na wakati huo kuruhusu maji kuingia na kutoka ndani yake huku kikizunguka juu ya maji. Ndani yake kuna bakteria spesheli wenye uwezo wa kusafisha maji kwa kutafuna (digest) chembechembe chafu zilizo kwenye maji (pollutants).
Kinachozaliwa baada ya tukio hilo ni Carbon Dioxide na umeme, umeme huo unatumiwa na roboti huyo kuendelea kufanya kazi. Na hivyo kutoitaji umeme wa ziada kamwe.
Mchoro unaoonesha ubunifu ulioenda kwenye utengenezaji wa roboti huyo

Mchoro unaoonesha ubunifu ulioenda kwenye utengenezaji wa roboti huyo

Ugunduzi na utengenezaji wa teknolojia hii unaonekana unaweza kutumika katika maeneo mbalimbali ya uchafuzi wa mazingira unaohusisha maji – hii inaweza ikawa kwenye mabwawa, mito na labda ata bahari uko mbeleni.

Je una maoni gani juu ya teknolojia hii na utumiaji wake?

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
SOMA PIA:  Dell XPS 15: Kompyuta nzuri kwenye uhariri wa picha/video
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

1 Comment

  1. Pingback: Row-bot: Fahamu Roboti Mdogo Anayesafisha Maji bila Kuitaji Kuchajiwa Kamwe | Teknolojia

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com