Saa ya kisasa isiyochajia na kitu chochote bali na joto la mwili wa binadamu

0
Sambaza

Katika kizazi cha teknolojia siku hizi kuna saa maarufu sana kwa jina lisilo rasmi la ‘saa janja’ zikiwa zimesheheni mengi mazuri yanayosaidia katika maisha ya kila siku yaliyozungukwa na teknolojia. Sasa kuna saa nyingine inaweza ikakufanya usitamani tena kuchaji kitu chochote daima.

Kwa muonekano unaweza ukadharau uwezo wake ila ukishajua kile ambacho kimewekwa ndani ya saa hii ya kisasa kabisa ndio utakubali kuwa kuna wakati utafika hata simu zetu hatutakuwa tunahitaji nishati ya umeme kuweza kuzichaji. Matrix PowerWatch imenivutia sana na kupelekea kuandaa makala hii ili niwafahamishe na wengi kuhusiana na saa hii.

Uchambuzi wa ndani kuhusu Matrix PowerWatch.

Haihitaji kuchajiwa. Hii ndio sifa kuu ya Matrix PowerWatch ambayo daima hutohitaji kuichaji kwani yenyewe inategemea nguvu kutoka kwenye joto la mwili wa binadamu; ukiivua inajizima lakini huku ikiwa imehifadhi data zako za kiasi gani mwili wako unazalisha nishati ya umeme na ukija kuivaa tu inawaka na kuendelea pale ilipokuwa imeishia.

Ina uwezo wa kukaa kwa miezi 12 bila kuishiwa na nguvu na ukija kuivaa tena itafanya kazi kama ilivyokuwa hapo awali.

>Ina hesabu kiasi cha calories ambacho mwili imetumia. Sote tunafahamu kuwa mwili wa binadamu unapofanya kazi calories huzalishwa kutokana na chakula tunachokula kila siku. Mwili unapofanya kazi na kutoka jasho hapo kuna kiasi cha calories kinakuwa kimetoka mwilini (asilimia kubwa kwa njia ya jasho) sasa Matrix PowerWatch inachofanya ni kuhesabu kiasi gani cha calories ambacho mwili wako umepoteza kwa siku.

Mwili wa binadanu huunguza calories na kugeuza kuwa chanzo cha nguvu ambazo nguvu hizo pia zitatumika kuifanya saa Matrix PowerWatch ifanye kazi. Pia, inafanya kazi ya kuhesabu hatua utakazotembea kwa muda wote ambao utakuwa umeivaa.

>Inafuatilia mwenendo wako wa kulala. Saa hii itakupa taarifa nyingi ya mwenendo wako pale unapokuwa usingizini na pale utakapoamka basi utaweza kuangalia na kujua mengi kuhusu unapokuwa usingizi; ni lazima uwe umeivaa saa hiyo ili iweze kufuatilia mwenendo mzima wa aliyopo usingizini.

SOMA PIA:  AzamTV App yapakuliwa zaidi ya mara milioni moja

>Haingii maji kwa umbali wa mita 50 kina cha maji. Saa hii (Matrix PowerWatch) ipo matoleo mawili na toleo la Matrix PowerWatch yenyewe haingii maji mpaka umbali wa kina cha mita 50 chini ya maji huku toleo la pili, Matrix PowerWatch X yenyewe haiingii maji mpaka urefu wa kina cha mita 200 kwenda chini ya maji.

Kwa waogeleaji wa kina kirefu hawawezi kuwa na hofu ya saa zao kuharibika kutokana na uwezo wa Matrix PowerWatch kuhimili kina cha maji hadi kina cha mita 50 kwenda chini.

>Inabadilika muokano wake kulingana na hisia za muhisika (kama mtu amefurahi/amekasirika). Ndio, kama mhusika atakuwa amekasirika basi Matrix PowerWatch itabadilika muonekano kulingana na vile utakavyokuwa kwa wakati huo.

Matrix PowerWatch: Muonekano wa saa utabadilika kulingana na mwili wako utakavyobadilika kutoka kwenye furaha hadi huzuni au mchovu mpaka mwenye nguvu, n.k.

>Matrix PowerWatch App. App ni itakueleza yote kuhusiana na kiasi cha nishati ambacho mwili wako kimezalisha kwa siku hiyo, kama unapata usingizi wa kutosha unapolala, kiasi cha calories ambacho mwili wako kimepoteza.

Taarifa hizi za kutoka kwenye Matrix PowerWatch App unaweza ukazisambaza kwa wengine waone mwenendo wa mwili wako. Matrix PowerWatch App bado haijaanza kupatikana ila inatarajia kuanza kupatikana hivi karibuni.

>Bei na matoleo. Matrix PowerWatch ipo katika matoleo mawili makuu, PowerWatch ambalo limeanza kupatikana mwezi huu wa Novemba kwa $169|Tsh. 380,250 na PowerWatch X litakaloanza kupatikana mwezi Desemba kwa $199|Tsh. 447,750. Lipo toleo moja maalum PowerWatch Black Ops ambalo limeanza kupatikana mwezi Novemba kwa $249|Tsh. 560,250.

SOMA PIA:  Ndege ya kwanza inayotumia umeme yarushwa China

Baada ya uchambuzi wa kina kuhusu Matrix PowerWatch unafikiri itakuwa imekidhi mahitaji ya wengi na kupelekea saa hizo kununuliwa kwa wingi? Tuandikie maoni yako hapo chini.

Vyanzo: Power Touch, Tough Gadget

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com