Sababu Kwa Nini SnapChat Ni Tishio Kwa Facebook!

0
Sambaza

Kwanza kabisa, soko la mitandao ya kijamii limekamatwa na mtandao wa kijamii wa Facebook. Mtandao huu ulitangazwa kuwa mkubwa kabisa mwaka 2009. Baada ya hapo miaka miwili baadae Snapchat ilikuja na mbwembwe ndio zikaanza.

Facebook mpaka sasa ina utajiri zaidi ya dola bilioni 30 za kimarekani wakati snapchat mpaka sasa ina utajiri wa dola bilioni 15 za kimarekani tuu.

Swala ambalo liko wazi ni kwamba mtandao wa Facebook siku hizi haulali kwa amani kama zamani kwani wanahofia mtandao huu wa Snapchat unaweza ukashika soko kuliko sana na tishio likazidi ongezeka. Hii inadhihirishwa dhahiri kwani hata mmiliki wa Facebook , Mack Zuckerberg alijaribu kuununua mtandao huu wa Snapchat – kama huwezi washinda, wanunue – zaidi ya mara mbili na mara zote hizo alikataliwa ombi lake.

Mbali na hapo facebook ilikuja na mkakati wa kuleta mitandao mingine ya kijamii inayofanana na Snapchat kama vile Poke, ambayo ilianzishwa mwaka 2012 na Slingshot, ambayo ilianzishwa mwaka 2014 lakini bado mbinu zote zimegonga mwamba.

Tofauti Kuu Kati Ya SnapChat Na Facebook Nii:

1. Utekaji Wa Wateja Wengi Sokoni
Snapchat imeliteka soko. Watumiaji wengi wa mtandao huo wapo ndani ya miaka 19 mpaka 24. Watumiaji ndani ya miaka hiyo ni zaidi ya asilimia 37 ya watumiaji wote wa mtandao huo. Kundi hili la watu wana asilimia kubwa ya kununua bidhaa mbalimbali katika mtandao huo kama vile lensi n.k ukilinganisha na kundi lingine lolote la umri. Licha ya hivyo kundi hilo linashiriki zaidi katika kutengeneza ‘Snaps’ (post) mabalimbali na nyingi zaidi kuliko kundi lingine lolote la umri.

Snapchat

Snapchat

2. Ubora Wa Muda Mfupi
Snapchat ina faida ya kuwa na ubora wa muda mfupi. Fikiria kitu kinakuwa bora sema kinakuwa na maisha mafupi, lazima utakimiss sio?. Kuna ukweli mkubwa juu ya hili ukijikita sana katika saikolojia ya mwanadamu, lakini hili sio watu wengi wanaliona. Thamani ya kitu inazidi kuwa kubwa kama kitu hicho kinakuwa na maisha madogo au kidogo. Ngoja nikupe mfano, kwa mfano mwanadamu angekuwa na uwezo wakuishi miaka hata 500 bila shaka watu wengi wangekuwa wamebweteka tuu na wasingekuwa wanaidhi maisha yao kama inavyotakiwa. Sasa turudi kwenye Snapcha, mtandao huu una picha na video ambazo zinajiua zenyewe kwa muda flani (siku moja) au baada tuu ya kusomwa. Kwa kifupi huwezi ukaingia katika mtandao huu na ukakuta taarifa au post ya juzi

SOMA PIA:  Instagram Yaja Na 'Sticker' Kama Snapchat!

Kutokana na hili watumiaji wa mtandao huu wamekuwa na hamasa kubwa ya kutumia mtandao huu. Pia watumiaji wana shauku kubwa ya kuona marafiki zao wametuma kitu gani – wasipokiona kwa muda huo wana hati hati ya kutokiona tena — na pia inamaanisha kuwa watu wanao ‘post’ vitu katika mtandao huu wana hati hati ndogo sana ya kujibana kwa kile wanachotuma katika mtandao.

3. Ishu Ya Matangazo
Matangazo katika mtandao wa kijamii wa Snapchat ni tofauti kabisa nay ale ambayo yanapatikana katika mtandao wa kijamii wa Facebook. Pia cha kujiweka katika hali ya utofauti kabisa mtandao huo una kurasa (page) moja ambayo inajumuisha matangazo yote. Jambo hili ni tofauti kubwa kulinganisha na mtandao wa Facebook ambao matangazo yake yantokea katika eneo la kawaida ambalo unaweza ona post za watu (News feed). Ukiwa facebook unavyozidi kushuka chini unazidi kuona post nyingi za watu, pia hapo utakuwa unazidi kuona matangazo mengi.

Ukurasa Wa Matangazo Ndani Ya SnapChat Maarufu Kama Discovery

Ukurasa Wa Matangazo Ndani Ya SnapChat Maarufu Kama Discovery

Sasa tukiabakia hapa kwenye swala la matangazo kumbuka kuna watu wengine ambao hawapendi kuona matangazo na facebook haijawaangalia hao. Kwa upande mwigine mtandao wa Snapchat umefanya hivyo na kuyaweka matangazo katika sehemu ambayo inajitegemea (tofauti na eneo ambalo unaweza ukaona post za watu).

SOMA PIA:  Facebook inafanyia majaribio kipengele kipya kutenganisha machapisho ya kawaida na yale ya kibiashara

Kila kampuni kubwa linakuwa kutokana na misingi yake mizuri iliyojiwekea katika soko. Hasa misingi ambayo itayatofautisha makampuni hayo na makampuni mengine. Kwa mfano Facebook na Twitter yote yamejikita katika mitandao ya klijamiii lakini ukifuatilia ni kwamba makampuni hayo yako tofauti kabisa.

Hapo awali Google walifeli vikubwa kwa kuanzisha mitandao kadhaa ya kijamii kama vile Google Plus ikiwa na lengo la kuipiku kampuni ya Facebook, lakini kwa kuwa kampuni hiyo ilisimama imara katika misingi yake bado inasonga mbele.

SOMA PIA:  Kigogo wa Google ajiunga na Facebook

Nakumbuka Siku kadhaa zilizopita nlikua napiga stori na Shamsa, Ahhh! Yule mwenye Tovuti ya maisha ya kila siku maarufu kama BintiEsque (www.BintiEsque.Com) na nikawa nampa tathmini yangu juu ya Teknolojia hasa hasa kwa mtandao wa Snapchat na nikaufananisha na mitandao mingine juu ya ukuaji wake n.k. Nna furaha kubwa leo ku ‘Share’ sababu hizi na wewe.

Kwa vitu hivi vitatu tuu nilivyoelezea kutoka katika mtandao wa kijamii wa Snapchat facebook wanahemea kooni. Sasa pata picha Snapchat wakiweza kujiboresha zaidi katika kuhakikisha wanaliteka soko . Wakifanya hivyo inaweza ikawa ni sikukuu kwao.

Niandikie sehemu ya comment hapo chini hili umelipokea vipi na ni nini maono yako juu ya jambo hili. Kumbuka kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKona kila siku. Pia Kumbuka TeknoKona Daima Tupo Nawe Katika Teknolojia!.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com