Sababu Kwanini Usinunue iPhone 6S Au 6S Plus ya GB 16!

0
Sambaza

Apple inaelekea kupata mauzo makubwa kutokana na bidhaa zake mbili zilizo njiani yaani iPhone 6s na 6s Plus. 6s hii itakuja na mabadiliko makubwa mawili kulinganisha na toleo lile la mwanzo.

Badiliko la kwanza ni Tachi skrini ya 3D (3D Touch screen) ambayo inatoa majibu kulingana na namna uliyoigusa (Ukigusa kwa nguvu, majibu haraka). Hii itakua imeleta mabadiliko makubwa sana katika ulimwengu wa simu janja.

Lakini kwa sasa TeknoKona inajikita katika badiliko lingine (la Pili) ambalo linaweza kuwa ni kikwazo kwako kama ukikimbilia kununua simu hiyo ya iPhone 6s. Kwa matoleo ya iPhone 6 hadi  6s Apple wameboresha uwezo wa kamera yaani kutoka 8 MP mpaka 12 MP na pia wameongeza kiwango cha pixels ambayo inaongeza ubora wa picha

image

Pia katika kuboresha picha kamera ya simu hiyo inakuja na vitu viwili vya nyongeza. Cha kwanza ni kwamba unaweza chukua video kwa kutumia mfumo wa 4K ambao pia unajulikana kama Ultra HD. Hii inapita simu zingine ambazo zinachukua video kwa mfumo wa 1080p.

Cha pili ni kipengele cha Live Photos.Wakati unabofya kioo cha simu yako (iPhone 6s) ili kuchukua picha, hautapiga picha fremu moja tuu bali utachukua sekunde 1.5 kabla na baada ya kubofya (kwa ujumla sekunde 3)

Baadae wakati unaangalia picha zako, ukibofya picha kwa nguvu itajicheza mfumo mzima wa kurekodi (zile sekunde 3) hii ikijumuishwa na sauti. Yaani hapa utaona picha zako mbalimbali zikija kwenye uhai — mfano utaona picha za mwanao zikiwa hai, hata zile zako na marafiki zako mkiwa maeneo —  Utaweza ona wakati wa kushangaza uliojitokeza kabla na baada ya kupiga picha hizo

INAYOHUSIANA  Simu za iPhone 6, SE, X hazitatengenzwa tena

image

Hivi vyote ni vipengele vinavyovutia sio? Lakini ili kuendana navyo kuna toleo moja si sahihi kulinunua

pros and cons of buying viagra online SOMA PIA: Apple watambulisha iPhone 6s na 6s Plus, Haya ndio ya kuyafahamu kuhusu simu hizo mpya

Apple wameamua kuzipa simu za iPhone 6s na 6s Plus GB 16. Miaka kadhaa iliyopita GB 16 ilikuwa ni uhifadhi mkubwa sana lakini kwa siku hizi si kitu kabisa. Fikiria ni vitu vingapi vinaigia katika simu yako kwa siku kama vile picha, voice notes, miziki, video kutoka whatsApp na sehemu zingine mbali mbali.

Mara tuu ya kujaza App za kutosha, Miziki, Video na picha katika iPhone 6s yako yenye GB 16 uhifadhi huo utaondoka na hii ndio maana watengenezaji wengine wa simu wameachana kabisa na kuzalisha simu zenye GB 16 na kendelea na zile za GB 32. Hata pia kwa maboresho haya yanayofanywa na Apple GB 16 bado kidogo tunaiaga.

buy clomid online bodybuilding Sasa Kwanini Usijipatie iPhone 6S ya GB 16!?

Video katika mfumo wa 4K inakuwa na ubora mara nne katika pixel zaidi ya mfumo ule wa 1080p (mfumo wa video wa zamani katika iPhone). Hii inamaanisha mfumo huu wa 4K unachukua chumba (uhifadhi) zaidi. Dakika moja ya kuchukua video katika mfumo wa 1080p ambayo ina fremu 30 kwa sekunde inatumia MB 67 mpaka MB 96 hii inamaanisha kwa ujazo wa GB 16 hapa utarekodi video yako kwa masaa tuu mpaka kujaa.

INAYOHUSIANA  Ulazima wa 'Redeem Code' kwenye rununu

Ukilinganisha na mfumo wa 4K. Dakika moja katika mfumo huu ni sehemu yeyote katika MB 270 mpaka 380 hii inamaanisha kwa ujazo wa GB 16 hapa unaweza kuchukua video chini ya lisaa. Na pia hapo fikiria kama huna kitu kingine chochote katika uhifadhi wa simu yako

Kumbuka pia kuna Live Photos, ambazo ni vivideo vifupi fupi na pia zina ‘Resolution’ kubwa kulinganisha na 4K video.Live Photos sio video za kawaida tulizo zizoea, Apple wamesema ni “Teknolojia ya kuchukua fremu hadi fremu” ambayo hiyo ni tofauti

Bado picha ambayo ina MP 12 itachukua ukubwa wa MB kadhaa, lakini  ‘kila picha’ ina MB kadhaa sio? inategemea tuu jinsi ilivyopigwa na wapi ilipopigwa.Kila ‘picha’ itakuwa na MB 10 au zaidi sasa kama ukipiga picha 100 katika mfumo wa Live Photos unaweza ukawa unatumia GB moja ya uhifadhi wa simu yako bila kugundua.

image

Ni kweli unaweza hamisha picha zako na video zako muhimu katika huduma ya Apple (iCloud) au hata huduma zingine ili  kujipatia juhifadhi wa kutosha katika simu yako. Lakini hii itakuchukua muda mrefu sana kupangilia kipi kipo kwenye iPhone na kipi kipo kwenye iCloud. Na pia kama itatokea utataka kuona picha zako zilizo katika iCloud katika simu (iPhone) yako itabidi uanze kushusha (download) picha hizo. Kama unatumia mtandao wa simu utamaliza data (Bando) zako mapema kwa mafaili hayo yatakuwa katika ujazo mkubwa.

INAYOHUSIANA  Mambo si shwari kwa baadhi ya iPhone

Kwanza ukiangalia hapa unaweza ukaona kama Apple vile wamefeli lakini ukija kuangalia vizuri katia tofauti za ujazo katika simu hizi za 6s ni kwamba kuna ujazo wa GB 16, GB 64 na GB 128 (unaweza kujiuliza GB 32 iko wapi).

Apple wangeweza kuifanya GB 16 kuwa GB 32 bila kuweka faida ya ziada lakini inaonekana kampuni hiyo inawasukuma watu kununua simu yenye ujazo mkubwa zadi yaani GB 64 na zaidi. Lakini hata hivyo mambo ya uhifadhi yanategemea na mtu mwenyewe mfano ukimpa iphone bi mkubwa wangu sijui kama atajaza hata hiyo GB 16 kwanza sijui kama ataweza tumia kabisa (uzee una tabu zake).

Tuambie kama ukifikiria kununua matoleo mapya ya iPhone 6s utafikiria kutoa pesa chache ili kupata ile ya GB 16 au utaongeza dau ili kwenda sambamba na ile ya GB 64 tuandikie jibu lako sehemu ya comment.Pia  Kumbuka matoleo haya ya 6s hayana ujazo wa GB 32. TeknoKona Tupo Nawe!

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply