Safaricom yapigwa faini ya mamilioni kwa sababu ya huduma mbovu

0
Sambaza

Safaricom yapigwa faini. Kampuni ya mawasiliano ya simu Safaricom nchini Kenya, imetozwa faini ya mamilioni ya fedha kwa sababu ya huduma mbovu.

Kampuni hiyo ilitozwa KSh. 270.1 milioni|Tsh. 7,290,000,000 na Mamlaka ya Kusimamia Mawasiliano nchini humo (CAK) katika kipindi cha mwaka uliokamilika mwezi Machi 2017.

safaricom yapigwa faini

Safaricom yapigwa faini: Nembo ya kampuni ya mawasiliano ya Safaricom

Mwaka jana, kampuni hiyo ilitozwa faini ya Sh. 157 milioni. Katika ripoti iliyozinduliwa mwishoni mwa wiki jana; kiwango hicho ni asilimia 0.15 ya mapato yote ya kampuni hiyo kabla ya kutozwa ushuru, Machi 2017.

SOMA PIA:  Jinsi Ya Ku'Log Out' Instagram Kwa Kutumia Kifaa Kingine!

Kampuni hiyo ilifuata kanuni kufikia asilimia 62.5, kiwango kilicho chini ya kiwango kilichopendekezwa cha asilimia 80. Safaricom iliimarika katika viwango vya utoaji huduma kutoka asilimia 50 mwaka jana, ongezeko la asilimia 12.5.

Baadhi ya masuala yanayozingatiwa na CAK kutokuwa na uwezo wa kumaliza mazungumzo kwa wateja na ubora wa sauti.

Nchini Tanzania tatizo la kukatika kwa mawasiliano baina ya mteja mmoja na mwingine imekuwa ni kitu cha kawaida pamoja na usikikaji mbaya wa sauti kwa watumiaji wa huduma za mawasiliano.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com