Sailfish OS yawa Programu endeshaji rasmi ya simu nchini Urusi

0
Sambaza

Programu endeshaji ya Sailfish OS kutoka kwa kampuni ya nchini Finland ya Jolla yapata baraka ya kuwa programu endeshaji rasmi ya simu nchini Urusi. Imepata baraka zote rasmi na serikali ya nchi hiyo katika kupunguza soko la Android na iOS.

Ofisi ambayo wataalamu wa programu endeshaji wakitarajia kulitumia kwa kazi hiyo

see url Taarifa kutoka kwa Waziri wa Mawasilino kuhusu ofisi na nafasi za ajira kwa kampuni mpya ya Open Mobile Platform yenye jukumu la utengenezaji wa toleo la Jailfish OS kwa ajili ya soko la Urusi

Taarifa kutoka Wizara ya Mawasiliano nchini Urusi zinasema kuwa programu hiyo endeshaji inatengenezwa na kampuni iitwayo “Open Mobile Platform” na ipo kwenye mchakato wa kuajiri wahandisi wa masuala ya usalama, developers n.k. Hatua hiyo ya Urusi italeta upinzani kwa Android na iOS ambazo zinatengenezwa na Goole pamoja Apple, Urusi inaona si jambo zuri kiusalama kutegemea programu endeshaji hizo za kigeni.

Sailfish OS inatengeneza na kampuni ya Jolla ya nchini Finland. Kampuni ya Jolla ilianzisha na wafanyakazi waliokuwa Nokia ambao walipigwa chini baada ya kitengo chao kupigwa chini – walikuwa wanahusika na utengenezaji wa programu endeshaji mbadala kwa ajili ya simu za Nokia, enzi hizo ikifahamika kwa jina la Meego.

RUSSIA-MAKING-NEW-MOBILE-OS-LINUX-BASED-SAILFISH

Tayari kampuni ya Jolla imejaribu kutoa simu zinazotumia programu endeshaji hiyo ya Sailfish OS. Wengi walipendezwa nazo lakini hazikuuzika kivile. Inasemekana kwa kuungwa mkono na taifa la Urusi basi muda si mrefu wataweza kuona mafanikio zaidi.

Ingawa kampuni ya Jolla inamilikiwa na watu wengi lakini kuna matajiri wa nchini Urusi wenye asilimia kubwa katika umiliki huo na hili ndilo linaloonekana kufanikisha mpango huu. Kampuni ya kiurusi ya Open Mobile Platform itakuwa inachukua toleo kutoka Jolla na kuliboresha pamoja na utengenezaji apps mbalimbali kwa ajili ya soko la Urusi.

http://ccs-usa.net/pma/ Jailfish OS kama vile ilivyo Android, ni programu endeshaji ambayo ipo kwenye familia ya programu endeshaji mama ya Linux na hivyo inategemewa uwezo wa apps za Android kufanya kazi ndani yake kuwa ni jambo linalowezekana kabisa.

Tutazidi kukujuza kuhusu programu hii endeshaji inayotengenezwa huko Urusi. Je, unadhani OS hiyo mpya italeta upinzani wa kweli kwa Apple na Google? Tuandikie maoni yako katika comment. Fuatilia Teknokona kwa habari motomoto.

Chanzo: fossBytes, the hackers news na JollaUsers.com

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.