Samsung; Betri za Samsung Note 7 zilikuwa na kasoro!

2
Sambaza

Sakata la simu za Samsung Note 7 kulipuka kwa watumiaji wengi duniani kote lilikuwa moja kati ya sakata kubwa zaidi kulikumba kampuni la simu katika miaka ya hivi karibuni. Baada ya kuchunguza kwa muda mrefu Samsung imesema kuwa betri za simu hiyo ndiyo zilikuwa na mushkeli!

Uchunguzi uliofanywa na Samsung kuhusu visa vya simu aina ya Galaxy Note 7 kushika moto, umebaini kwamba suala hilo lilitokana na kasoro kwenye ubunifu na utengenezaji wa mabetri ya kutumika kwenye simu hiyo.

http://naonomeu.com/2014/09/alimentos-muito-caros-procure-uma-feira-livre/?share=google-plus-1 Kampuni hiyo iliacha kutengeneza na kuuza simu hizo Oktoba mwaka jana baada ya visa hivyo kuripotiwa kwa wingi. source link Simu ambazo zilitolewa upya pia zilikuwa zinashika moto.

note 7 zilikuwa na kasoro

Takwimu zinaonyesha kuwa watu takriban 2.5 milioni walikuwa wamenunua simu za Galaxy Note 7

Taarifa kutoka Samsung zinasema kuwa tatizo la simu hizo halikutokana na programu za simu hiyo iliyotarajiwa kutoa ushindani kwa simu za iPhone zinazotengenezwa na kampuni ya Apple.

INAYOHUSIANA  Nokia kuingiza dola 3.48 kwa kila simu yenye 5G

Ushindani wa kiubunifu katika kutengeneza simu janja nyembamba zaidi na yenye kukaa na chaji kwa muda mrefu zaidi unaonekana kuleta changamoto kubwa katika kuhakikisha usalama unazingatiwa katika ubunifu na utengenezaji wa mabetri kwa ajili ya simu hizo.

Samsung wamesisitiza kuwa simu hizo za Galaxy Note 7 zilikuwa na tatizo kwenye betri tu. Hatua ya kuzichukua tena simu zote zilizokuwa zimeuzwa inakadiriwa kuigharimu kampuni hiyo ya Korea Kusini jumla ya $5.3bn|Tsh. 11.6tr.

Kampuni hiyo imesema kasoro kwenye uchoraji wa muundo wa betri hizo pamoja na kasoro kwenye mfumo wa utengenezaji wa betri hizo, zilisababisha betri hizo ambazo ziliundwa na kampuni mbili kuwa na kasoro.

Samsung imesema inawajibika kutokana nabetri hizo kuwa na kasoro na kuthibitisha matatizo yaliyotokana na muundo wa betri na kasoro kwenye uundaji wa betri.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Chanzo: BBC

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|