Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge Kuanza Kupata Toleo la Android 6.0.1 Marshmallow - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge Kuanza Kupata Toleo la Android 6.0.1 Marshmallow

0
Sambaza

follow Habari nzuri kwa watumiaji wa simu za Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge kwani muda si mrefu wataweza kupata msasisho (update) wa Android 6.0.1 Marshmallow.

Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge

Galaxy S6 na S6 Edge ndizo simu mpya moto zaidi kutoka Samsung kwa sasa

Kwa sasa kampuni hiyo ishaanza kuanza kutoa msasisho huo wa toleo jipya kabisa la Android kwa watumiaji wa Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge wa nchini Korea kusini. Kwa mara nyingi kampuni ya Samsung huwa inaanza kutoa masasisho katika taifa hilo ambalo ndio nyumbani kwao.

Ingawa badi hawajatoa ratiba rasmi ila ni kawaida ya masasisho kuanza kusambaa kwa watumiaji wa mataifa mengine wiki kadhaa baada ya watumiaji wa nchini Korea Kusini kupata masasisho.

INAYOHUSIANA  Motorola wametoa nyingine inaitwa Moto Z3

Kuanza kutoa masasisho katika nchi moja tuu huwasaidia kuona matatizo na kuyarekebisha kabla ya kuanza kuyasambaza kwa watumiaji wa simu husika duniani kote.

Ni nini kipya kwa toleo la Android 6.0.1 Marshmallow kwa watumiaji wa Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge?

Haya ni baadhi ya kuyatarajia…

Soma Pia – Uchambuzi wa Samsung Galaxy S6 na Galaxy S6 Edge

INAYOHUSIANA  Jinsi ya kuficha au kufichua mazungumzo kwenye WhatsApp

Kama wewe ni mtumiaji wa simu hizi basi endelea kuwa na subira na muda si mrefu kupitia eneo la ‘Update’ kwenye simu yako utaweza kuona mualiko wa kusasisha (update).

Vyanzo: Mbalimbali mtandaoni

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply