Samsung Galaxy S8 kufunikwa na kioo (display) kwa asilimia kubwa zaidi

Samsung Galaxy S8 kufunikwa na kioo (display) kwa asilimia kubwa zaidi

0
Sambaza

Habari za chini kwa chini kulingana na ripoti iliyotolewa Jumatatu hii nchini Korea Kusini inasemekana toleo lijalo la simu maarufu za familia ya Galaxy kutoka Samsung, Galaxy S8, itafunikwa kwa asilimia kubwa na kioo chake (screen/display) kuliko simu nyingine yeyote iliyokwisha ingia sokoni.

http://blog.hearthstonegrill.com/wp-json/oembed/1.0/\

Ripoti hiyo iliyotolewa na shirika la The Investor la nchini Korea Kusini, limemkariri mhandisi (engineer) wa kamapuni ya Samsung kitengo cha kioo (display) bwana Park Won-sang akisema toleo la Samsung Galaxy S8 linatafunikwa kwa mbele kwa asilimia 90 na ‘display’.
http://msdubindesign.com/category/new-website/ Kulingana na tovuti ya habari ya CNET kwa sasa wastani wa eneo la mbele linalofunikwa na kioo (display) kwenye simu zilizopo sokoni kutoka makampuni yote ni asilimia 80 tuu.
Mhandisi huyo huyo alikaririwa akisema ya kwamba lengo la Samsung si kuishia kwenye asilimia 90 tuu. Tutegemee kuona matoleo ya simu zijazo kutoka kwao kuzidi kufunika eneo kubwa la mbele la simu na display.

buy discounted Lamictal online Hii si mara ya kwanza kwa habari kuhusu toleo hilo la simu linalotegemewa hapo mwakani kutambulishwa rasmi kuhusisha ujio wa simu hiyo kuwa itakuwa display imefunika zaidi eneo la simu hiyo.

INAYOHUSIANA  Uhalifu wa mitandaoni unazidi kudhibitiwa

Inategemewa eneo la kubonyeza kwa ajili ya kwenda ‘Menu’ n.k ambalo limekuwa eneo la chini kwa kati muda mrefu litaondolewa na eneo hilo lote kufunikwa na kioo cha display. Inategemewa kupitia kioo cha display eneo la chini teknolojia ya kutambua alama za vidole ‘fingerprint sensor’ itawekwa ndani yake.

Tutaendelea kukuletea habari za Samsung Galaxy S8…tetesi na taarifa rasmi kama vile tutakavyokuwa tunazipata.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.