Samsung Galaxy S8 na S8 Plus: Zifahamu simu mpya kutoka Samsung! #Uchambuzi - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung Galaxy S8 na S8 Plus: Zifahamu simu mpya kutoka Samsung! #Uchambuzi

3
Sambaza

Samsung wametambulisha rasmi simu mpya ya Samsung Galaxy S8 na S8 Plus. Kwa kiasi kikubwa ule ushindani na ubishi wa kwamba kati ya simu za iPhone na simu za Galaxy nani bora umekwisha hapa. Samsung wamefanya kweli.

go to site

Samsung galaxy s8

buy cheap Keppra Simu ya Samsung Galaxy S8

buy cheap diflucan Katika ubunifu na utengenezaji wa Samsung Galaxy S8 na S8 Plus Samsung wameenda mbali zaidi kuhakikisha simu hii ni ya kipekee dhidi ya simu zingine zote zilizopo sokoni kwa sasa.

Muonekano wa OS – Inakuja na toleo la Android Android 7.0

Samsung Galaxy S8 S8Plus

Simu za Samsung Galaxy s8 na S8 Plus zitakuja kwenye rangi mbalimbali

Vitu vizuri vya kitofauti vilivyofanyika katika simu hizi;

Screen (Kioo/Display yake)

Simu za Samsung Galaxy S8 na S8 Plus zinakuja na teknolojia mpya ambayo Samsung wameiita Infinity Display. Kioo chake kimekuja kupinda pande za kushoto na kulia mwa simu. Galaxy S8 inakuja na inchi 5.8 wakati S8 Plus ina kioo/siplay ya inchi 6.2.

Display zake zinatumia teknolojia ya SuperAMOLED, na kiwango cha juu ya HD – QuadHD (2960X1440)

Wembamba wake

Simu za SAMSUNG GALAXY S8 PLUS

Unapata msaidizi – Bixby Virtual Assistant

Kuwa na app yenye uwezo wa kukushauri na kufahamu mambo mbalimbali unayoyafanya katika simu imekuwa ni eneo ambalo kila kampuni ya simu inahakikisha inawekeza kwa sasa. Apple wanayo inaitwa Siri na Google pia wanayo ya kwao na sasa Samsung wamewekeza zaidi. Kwao anaitwa Bixby, huyu ni msaidizi atakayeweza kukuambia juu ya vitu mbalimbali, yaani unaweza piga picha ya kitu na Bixby atakuambia mambo mbalimbali kuhusiana na kitu hicho.

INAYOHUSIANA  Umoja wa Ulaya kudhibiti gharama za simu

Unaweza uliza kuna migahawa gani mizuri na moja kwa moja app hii itakupa taarifa za migahawa mizuri karibu nawe – ata bila ya kutaja eneo ulilopo… itafahamu.

Zinakuja na prosesa za kisasa zaidi

Matoleo ya Galaxy S8 na S8 Plus yatakuja na prosesa za Qualcomm Snapdragon 835 na pia kuna simu zitakazokuja na prosesa za Exynos 8895. Prosesa zote ni za kisasa zaidi, hivyo simu zitafanya kazi kwa kasi zaidi na tena bila kutengeneza joto zaidi.

Salama dhidi ya maji na vumbi

Simu zote zinaweza himili kiwango kikubwa cha vumbi na pia kulowanishwa na maji (waterproof).

Simu za kwanza kuja na Bluetooth 5

Simu hizi zimekuwa zimu za kwanza kabisa kuja na toleo jipya la teknolojia ya ya Bluetooth 5. Toleo hili jipya la teknolojia hii inawezesha utumaji wa mafaili haraka zaidi na pia vifaa kama vile spika za bluetooth zinafanya kazi wa ubora na kiwango cha juu zaidi.

INAYOHUSIANA  Vodacom na wizi wa fedha mtandaoni

Utumiaji mzuri zaidi wa teknolojia za utambuzi wa macho (IRIS scanner) na utambuzi wa sura (face recognition)

Ingawa teknolojia hizi zipo tayari kwenye simu nyingi za kisasa ila Samsung ndio wameboresha matumizi yake kwa kiasi kikubwa zaidi.

Utaweza kufunga na kufungua simu, pia utaweza kufunga baadhi ya apps kwa kutumia teknolojia hizo. Nje ya hizo bado pia simu inakuja na teknolojia ya alama za vidole (fingerprint scanner), hivyo utaweza kuchagua teknolojia ya kuitumia kwenye masuala ya ulinzi wa data zako upendavyo wewe.

Sahau ujazo wa GB 32, sasa ni kuanzia GB 64

Na kuanzia matoleo haya ya simu za familia ya Galaxy S matoleo yenye diski ujazo wa GB 32 ndio mwisho wake. Kuanzia Galaxy S8 na S8 Plus ujazo wa chini wa kuanzia ni GB 64.

INAYOHUSIANA  Ondoa vitu kwenye Thumbnails kuongeza nafasi

Unaweza itumia kama kompyuta

simu samsung galaxy s8 s8 plus

Simu ya Samsung Galaxy S8 ikiwa inatumika kama kompyuta

Upo hapo? Simu hii ikiunganishwa na display kama vile TV pamoja na kipanya na keyboard kwa kutumia teknolojia ya bluetooth utaweza kuitumia kama kompyuta.

Mengine…

Kamera mbili za MP 12 na moja ya Megapixel 8 kwa selfi. RAM ya GB 4. Betri ya mAh 3000 kwa toleo la S8 na mAh 3500 kwa toleo la S8 Plus. Pia simu inakuja na teknolojia nyingine mbalimbali za ambazo toleo lake la nyuma pia zilikuwepo kama vile VR, uwezo wa kuchaji wa bila ya kutumia waya n.k.

Bei ya Samsung Galaxy S8 itacheza kwenye Tsh 1,600,000/= wakati Galaxy S8 Plus itacheza kwenye takribani Tsh 1,840,000/=. Zitaanza kupatikana mwezi wa nne mwaka huu.

Kipi kimekuvutia zaidi?

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |