Samsung Kuleta Simu Zenye Betri ya Kukaa na Chaji Muda Mrefu Zaidi

0
Sambaza

Kampuni ya Samsung kupitia kitengo chake cha utafiti wamefanikiwa kupata teknolojia itakayohakikisha betri zinatengenezwa zikiwa na uwezo wa kukaa na chaji kwa kiwango kikubwa zaidi kulinganisha na za sasa. Simu za Samsung zenye kiwango kikubwa zaidi cha ujazo wa chaji katika betri ni pamoja na simu za Galaxy Note, mfano Galaxy Note 4 ina kiwango cha betri yenye uwezo wa kuifadhi chaji wa 3220mAh.

Kupitia teknolojia hii mpya bila kuongeza ukubwa wa mabetri, betri hizo zitaweza kuwa na uwezo wa kuhifadhi chaji wa hadi kufikia mAh 6,000, kiwango ambacho ni mara mbili ukilinganisha na mabetri yaliyopo sasa hivi. Kwa kiwango hichi kuna uwezekano mkubwa wa simu janja nyingi kuweza kutumika kwa zaidi ya siku mbili bila ulazima wa kuzichaji.

SOMA PIA:  Afrika yapata utambulisho wake(".africa") baada ya miongo mitatu

Soma Pia – Betri Inayojaa ndani ya Sekunde 60!

airtel tanzania bando

Tegemea betri za kukaa muda mrefu zaidi bila kuwa na ukubwa mkubwa zaidi wa kimuonekano.

Tegemea betri za kukaa muda mrefu zaidi bila kuwa na ukubwa mkubwa zaidi wa kimuonekano.

Ingawa teknolojia ya simu imekua kwa kiasi kikubwa bado teknolojia ya betri inayotumika katika betri hizi za lithium haijabadilika sana, bado inafanana kama ilivyoletwa na kampuni ya Sony katika miaka hiyo ya tisini. Kupitia teknolojia hii Samsung wataweza kuongeza kiwango cha ubora wa betri hizo pamoja na uwezo wa kiwango kikubwa zaidi cha chaji.

SOMA PIA:  Kuna uwezekano wa utumiaji simu gizani kusababisha upofu! #Utafiti #Afya

Soma Pia – Jinsi Ya Kufanya Betri Ya Simu Kuwa Na Maisha Marefu !!

Katika miaka miwili mitatu inayokuja inategemewa betri hizi zitaanza kutumika katika simu zake mpya ila pia kuna uwezekano mkubwa teknolojia hii ikaisaidia Samsung kwa kiasi kikubwa katika eneo la betri za magari ya kutumia umeme.

Soma Pia – Mambo 6 Yasiyo ya Kweli kuhusu Kuchaji Simu

Habari zinazidi kuwa nzuri kwa watu wasiopenda suala la kuchaji chaji simu, tunazidi kuona makampuni mengi zaidi yakiwekeza katika kuboresha teknolojia ya betri. Endelea kutembelea mtandao wako namba moja kwa habari na maujanja ya kiteknolojia katika lugha ya kiswahili.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. – Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom

| mhariri@teknokona.com |

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com