SAMSUNG Kutengeneza Simu ya Kukunja (flip phone) Tena

0
Sambaza

Imegundulika kwamba Samsung wanao mpango wa kutengeneza simu ya kukunja yaani Flip phone hivi karibuni. Hii ni aina ya simu yenye muundo wa kukunjika ambao ulikua maarufu sana kabla ya ujio wa simu janja.

Samsung wamekwisha pata kibali kutoka mamlaka husika juu ya utengenezaji wa simu hii ambayo imepewa jina la SM-W2016 kwa sasa.

Muonekano wa Samsung SM-W2016

SM-W2016 ina mgongo wa kioo na pembeni inaelekea kufanana na S6 Edge huku ikiwa na screen mbili za inchi 3.9 na resolution yake ni ndogo kuliko ile ya S6 edge. Pengine simu hii itakuwa nzito kidogo ukiringanisha na simu nyingi zilizopo sokoni kwa wakati huu ila itakuwa na 3GB RAM na nafasi ya 64GB kwa matumizi.Ikitumia mfumo endeshi wa Android 5.1 (lollipop).

SM-W2016 itakuwa inabeba kamera mbili moja nje na nyingine ndani, ya nje itakuwa na 8MP/1080p wakati ile ya ndani kwaajiri ya selfie ikiwa na 5MP. Pia simu hii itabeba keypad za kubonyeza(ya aina ya T9) kitu ambacho sio cha kawaida kwa simu janja nyingi,

SOMA PIA:  Google kuacha kutoa masasisho kwenye simu janja mbili!

Kama hii simu itasambazwa katika masoko yote (samsung walishawahi tengeneza “flip phone” ila wakaiuza soko la Korea Kusini pekee) basi tutarajie inaweza kufanya vizuri katika soko, hii  inatokana na ukweli kwamba kuna watu wengi ambao wanapenda keypad za kizamani na pia simu hii sio kubwa sana hivyo inaweza kubebwa mfukoni kirahisi kushinda simu nyingi zinazofanya vizuri katika soko.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com