Samsung kuanza kuuza simu zao Zilizokwishatumika(refurbished) kwa bei nafuu - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung kuanza kuuza simu zao Zilizokwishatumika(refurbished) kwa bei nafuu

1
Sambaza

Inasemekana kampuni ya Samsung Electronics Co Ltd inakuja na mpango wa kuuza simu zilizotumika na kisha kufanyiwa maboresho/kurekebishwa matatizo.

http://sodermpc.com/tag/skin-cancer-in-lawrenceville-ga/ Chanzo cha taarifa hiyo ni mfanyakazi wa ndani wa kampuni hiyo ambaye amelitonya shirika la habari la kimataifa la Reuters.

samsung galaxy s7

go Inategemewa simu za familia ya Samsung Galaxy ndio zitakazopatikana katika mpango huo.

Kampuni kama Apple tayari wanafanya hivyo hasa hasa katika nchi zilizoendelea.

http://brittanylowelegal.com/edit?url=https://mdpr.jp/news/detail/1667488 Inakuwaje hasa;

  • Samsung ina mfumo wa usajili unaoruhusu watu kujiandikisha katika mpango wa kununua toleo jipya la simu zao kila mwaka, huku mnunuaji akirudisha simu aliyokuwa anaitumia na kisha kuongeza pesa kidogo na kupewa toleo jipya la kisasa zaidi.
  • Pia kuna simu zilizonunuliwa na kuwa na tatizo na hivyo wanunuaji kubadilishiwa na kupewa mpya – simu za namna hii nazo zitatengenezwa na Samsung na kisha kuwekwa kwenye mauzo ya bei nafuu pia
  • Kwa muda mrefu simu hizi wamekuwa wakizichukua na hakuna aliyekuwa anajua kinachofanyika baada ya hapo
  • Kwa sasa simu hizo zitakuwa zinafanyiwa maboresho kama vile kubadilishwa ‘housing’ na betri na kisha kuuzwa kwa bei nafuu.

Uamuzi huu unategemewa kuongeza mapato kwa kampuni hii ambayo tayari inafanya vizuri.

Apple huwa wanauza simu za namna hiyo kwa bei ya takribani asilimia 60-69 ya bei ya mpya. Inategemewa kupitia mpango huu basi mtu ataweza kununua kutoka Samsung simu zile za hadhi ya juu, Galaxy, kwa takribani nusu ya bei yake ndani ya mwaka mmoja tokea toleo husika lianze kuuzwa.

Wengi wanategemea Samsung kuuza simu hizo hadi kwenye mataifa yanayoendelea kiuchumi ili kuweza kupambana na simu zingine za hadhi ya juu za bei nafuu kutoka makampuni kama Huawei, Tecno na wengine.

Vyanzo: Reuters na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Bakhresa aanzisha kampuni ya mawasiliano ya simu-Azam Telecom
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |