Samsung kuweka wazi ripoti ya uchunguzi juu ya milipuko ya Galaxy Note 7.

0
Sambaza

Imesemekana kwamba Samsung wanataweka ripoti ya uchunguzi juu ya nini hasa kili sababisha simu za Galaxy Note 7 ziwe zinashika moto.

Galaxy Note 7

Samsung haitausahau mwaka 2016 kamwe baada ya simu yake ya Galaxy Note 7 ambayo iliyozinduliwa na kampuni hiyo kugeuka mkuki katika moyo wa kampuni hiyo baada ya simu hizo kuanza kuwaka moto zikiwa zinatumiwa jambo ambalo lilipelekea simu hizo kuondolewa sokoni na kuipa kampuni hiyo hasara kubwa.

Simu ya Galaxy Note 7 kipindi ilipozinduliwa ilipewa sifa kubwa za kuwa ni moja ya simu janja bora zaidi kutoka mwaka 2016 —-lakini sifa hii ilidumu muda mchache baada ya matatizo ya milipuko ya betri kuanza kutokea.

SOMA PIA:  Infinix Zero 5 Pro: Simu janja mpya yenye kukaa na chaji siku mbili

Bado haijajulikana hasa ni kwanini simu hizi zilikumbwa na tatizo hilo, mwanzoni Samsung walidhani ni betri lakini hata baada ya kubadili betri bado simu hizo zili endelea kulipuka.

Galaxy Note 7

Ni muhimu sana kwa Samsung kuwaambia wateja wake ni nini kilitokea katika sakata hilo la Galaxy Note 7 ili iweze kurudisha imani ya watumiaji wake.

Sakata hili la kulipuka kwa simu hizi lilipelekea hasara kubwa kwa kampuni ya Samsung, bado hakuna taarifa halisi za hasara ila inategemewa kwamba kampuni hiyo ita poteza walau dola za kimarekani bilioni 5.1

SOMA PIA:  Google na Microsoft waungana katika vita dhidi ya mitandao ya mafaili ya wizi

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com