Kampuni ya Samsung imetangaza hivi karibuni itajiunga na orodha ya makampuni machache ambayo yamezindua memori kadi (microSD) yenye ukubwa wa 512GB.
Mpango wa kuzindua memori kadi yake ya ukubwa huo umesemwa na Mkurugenzi Mtendaji wa masoko, Drew Blackard wakati wa uzinduzi wa simu mpya ya Samsung galaxy Note 9.
Ingawa simu nyingi za kisasa zinaruhusu kuweka memori za ukubwa wa 512GB mpaka 1TB lakini ukweli memori kadi za ukubwa huo zipo chache mno kwa sasa katika soko.