Samsung Note 7 zitakazouzwa tena zitakuwa na kiwango kidogo cha betri

0
Sambaza

Mtandao mmoja maarufu kwa kupata habari na taarifa za siri kuhusu simu zilizokwenye matengenezo wamefanikiwa kupata picha inayoonesha simu ya Samsung Note 7 ikiwa inatumia betri la ujazo wa chaji ukilinganisha na mabetri yake rasmi.

samsung galaxy note 7

Kama unafuatilia makala zetu kwa makini basi utakumbuka ni wiki chache tu zilizopita tuliandika kuhusu simu za Samsung Note 7 kuuzwa tena hapo baadae, tena kwa bei pungufu hili ni baada ya Samsung kuonekana kufanikiwa kutatua tatizo na chanzo cha simu hizo kulipuka katika matumizi – tatizo lililofanya simu hizo kuondolewa sokoni miezi michache tuu baada ya kuingizwa tena kwa mafanikio mwaka jana.

SOMA PIA:  Samsung Galaxy S8: Samsung watengeneza simu rahisi zaidi kuvunjika kisha waitengenezea kikava

Zilivyoingizwa sokoni simu hizi zilikuwa zinatumia betri la mAh 3500 ila inaonekana zitakaporudishwa na kuanza kupatikana tena zitakuja na betri la mAh 3200. Hii si tofauti kubwa sana ila kikuu hapa ni kwamba upunguzaji huu umesaidia kupunguza mzigo kwa betri ambayo tayari ni nyembamba sana kutokana na ubunifu wa simu.

Pia toleo la Samsung Note 7 lililoingia sokoni lilikuwa linatumia toleo la Android 6.0 ila katika simu ambayo picha zake zimevuja mitandaoni zinaonesha kwa sasa Note 7 hizo zinatumia toleo la Android 7.0

SOMA PIA:  ZTE Axon M: Simu yenye screen mbili, ni simu inayoenda kinyume na tulichozoea

Vyanzo vingi vimeonesha simu hiyo itaanza kupatikana tena nchini India na Vietnam, ata picha iliyovuta chanzo chake ni tovuti moja nchini Vietinamu. Tayari Samsung wanakiwanda na wanatengeneza vitu vingi tayari kupitia Vietnam na hivyo haitashangaza kama wakianza kuuzia simu hizo nchini humo.

Simu za Samsung Note 7 zishalipuka na kusababisha hasara katika sehemu mbalimbali, gari hili aina ya Jeep liliungua nchini Marekani pale mwenye gari alipoacha simu yake ikiwa inachaji ndani ya gari hilo

Kuhusu upatikanaji wa simu hizo katika mataifa mengine ni hakika itachukua muda kidogo na itahusisha kupata vibali vipya kwa serikali nyingi ambazo tayari vyombo vyao vya usalama wa watumiaji vilishapiga marufuku uuzwaji wa simu hizo. Samsung watakuwa na kazi ya kuonesha simu hizi ni salama kwa sasa, hili halina shida sana kwani tayari Samsung waliwekeza katika moja ya taratibu bora zaidi kwa sasa za kupitia ubora na usalama wa betri na simu hii ni baada ya majanga ya Samsung Note 7 mwaka jana kutokea.

SOMA PIA:  Simu Janja binafsi kupigwa marufuku kwa wafanyakazi wa White House

Soma pia;

Tutaendelea kufuatilia ujio wa simu hizi sokoni tena. Je unadhani utakuwa tayari kutumia simu hizi kama zitauzwa kwa bei nafuu wako?

Vyanzo: Mitandao

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com