Samsung wabeba prosesa zote za kisasa za Snapdragon 835 kwa ajili ya Galaxy S8

Samsung wabeba prosesa zote za kisasa za Snapdragon 835 kwa ajili ya Galaxy S8 – wengine wazikosa

0
Sambaza

Kulingana na tovuti ya Forbes inasemekana kampuni ya Samsung imehakikisha imechukua oda zote za prosesa ya kisasa zaidi ya Snapdragon 835 zinazotengenezwa na kampuni ya Qualcomm kiasi ya kwamba washindani wake itabidi watumie prosesa za matoleo yaliyopita kwenye simu zao mpya.

get link snapdragon 835

http://colourway.co/product/navy-sweatshirt/ Prosesa ya Snapdragon 835 ni moja ya prosesa ya kisasa zaidi kwa sasa na simu nyingi za kisasa zinazokuja kutoka makampuni mengine mengi nguli zilitegemewa zitumie prosesa hizo – ila kutokana na Samsung kuweka oda kubwa ina maanisha wengine kama vile LG na HTC waliokuwa na lengo la kuweka prosesa hiyo kwenye simu zao kisasa kutumia prosesa toleo la nyuma (Snapdragon 821).

INAYOHUSIANA  Uzinduzi wa Samsung Galaxy Note 9 umefanyika

Simu ya Samsung Galaxy S8 inategemewa kutambulishwa rasmi mwezi wa nne mwaka huu nchini Korea Kusini. Utumiaji wa prosesa hii ya kisasa utaifanya simu ya Samsung Galaxy S8 kuwa moja ya simu zenye kasi kubwa zaidi sokoni.

follow Qualcomm ni moja ya kampuni nguli katika utengenezaji wa malighafi (‘parts’) mbalimbali muhimu zinazotumika kwenye vifaa vya elektroniki kama vile simu janja na kompyuta.

Simu za familia ya Galaxy S ni moja ya matoleo ya simu yanayoletea Samsung mapato makubwa sana katika biashara ya simu janja – ukujumlisha pia na simu za familia ya Galaxy Note.

Utumiaji wa prosesa hii ya kisasa utaifanya simu ya Samsung Galaxy S8 kuwa moja ya simu zenye kasi kubwa zaidi sokoni.

Tutaendelea kufuatilia ujio wa simu za Galaxy S8, endelea kuwa nasi.

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.