´╗┐ Samsung S8 Lite haipo mbali kuletwa kwenye soko - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung S8 Lite haipo mbali kuletwa kwenye soko

1
Sambaza

Kwa mujibu wa taarifa za kuaminika imeelezwa kuwa Samsung wanataka kuleta simu janja mpya ikiwa ni muendelezo wa kutoa simu ambazo zinatoka kwenye familia moja, Samsung S8 Lite ipo njiani kutambulishwa.

http://summerhouse.co.uk/bso-seasonal-brochure/

go Methocarbamol online canada Ni mwaka jana tu, 2017 Samsung walileta simu janja za S8 na S8 plus sasa ni wakati wa bidhaa nyingine kuja ili kuongeza kasi ya ushindani na kuwafurahisha wapenzi wa simu janja za Samsung. Unajua Samsung Galaxy S8 Lite itakuwa na sifa gani? Fuatilia pamoja nasi:

Prosesa/Ukubwa (ubora) wa kioo.

Hapa unaweza ukashangaa lakini ndio ukweli wenyewe, simu ya Samsung Galaxy S8 Lite itakuwa na prosesa ya Snapdragon 660 wakati S8/S8+ zina Snapdragon 835. Ukubwa wa kioo ni sawa tu mtangulizi wake, ina inchi 5.8 lakini pia ubora wa muonekano wa vitu kwenye kioo ni 2220x1080p huku kwenye S8 zote mbili ubora picha ni 2960x1440p.

Diski uhifadhi/RAM.

Simu ya Samsung Galaxy S8 Lite inakuja na diski uhifadhi wa GB 64 pamoja na RAM ya GB 4. Kwa kiwango hicho cha RAM pamoja na ukubwa wa nafasi ya kutunza vitu kwenye simu suala zima la simu kukwamakwama wkati inapofanya kazi itakuwa ngumu kidogo ila si kwamba halitowezekana.

Samsung S8 Lite

Rangi ya kuvutia kwenye Samsung Galaxy S8 Lite.

Betri/Rangi.

 Samsung S8 Lite itakuwa na betri yenye 3000mAh na kama kawaida ya simu nyingi betri lake halitoki. Kwa taarifa zilizovuja zinaeleza kuwa simu hii (S8 Lite) itakuwa katika rangi mbili; Nyeusi na Nyekundu isiyokolea.

INAYOHUSIANA  WhatsApp kupambana na taarifa za uongo

Kamera/Programu endeshi.

Inategemewa kuwa Samsung Galaxy S8Lite intakuwa na kamera moja nyuma nyenye MP 16 na ile ya mbele itakuwa na MP 8. Kuhusu programu endeshi, S8 Lite inaaminika kuwa itakuja na toleo la Android 8 maarufu kama Oreo.

Samsung S8 Lite

Muonekano wa nyuma wa Samsung Galaxy S8 Lite inayoonekana kuwa na kamra moja tu nyuma.

Hizo ndio sifa zake kwa uchache huku ikitegemewa kuzinduliwa Mei 21 huko nchini Uchina. Na kiujumla sifa za S8 Lite ndio maana halisi ya neno “Lite“; ni lazima isiwe bora sana kuzidi yule aliyetangulia.

Vyanzo: Tech Spot, Gadgets 360.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|