Samsung waendelea kuongoza mauzo ya simu soko la kimataifa #Ushindani - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung waendelea kuongoza mauzo ya simu soko la kimataifa #Ushindani

0
Sambaza

Kampuni ya simu za Samsung imeendelea kuongoza katika soko la kimataifa la simu duniani mpaka kufikia mwezi Aprili huku simu zinazozalishwa Uchina zikipata nafasi za juu katika soko kwa mwaka 2018.

go to link

Kwa mujibu wa kampuni ya utafiti ya StatCounter simu za Samsung zimepanda kwa asilimia 0.1; order clomid overnight Februari 2018 Samsung waliuza simu zao kwa asilimia 31.9 ukilinganisha na Februari 2017 ambapo waliuza asilimia 31.8 kwa simu zote zilizouzwa katika masoko ya dunia.

Samsung waendelea kuongoza

http://selectinteriordesign.com/wp-content/themes/enigma-premium/photobox/ link.href / Kwa miaka mingi tu bidhaa za Apple zimekuwa zikiongoza kimauzo lakini hivi karibuni takwimu zinaonyesha watu kupendezwa zaidi na bidhaa za Samsung hivyo kumtoa Apple kwenye nafasi ya kwanza kimauzo.

Apple imeendelea kuwa nafasi ya pili kwa kuchangia soko la simu janja kwa kuuza kwa asilimia 20.1 kwa mwezi Februari. Mwezi Januari 2018, Apple waliuza kwa asilimia 19.6 na iujumla mauzo ya bidhaa za Apple mauzo yake yamepanda kwa asilimia 0.5.

Washindani wengine.

Huawei imeshika nafasi ya tatu duniani kwa mauzo ya simu janja kwa soko la kimataifa baada ya mauzo yake kupanda kwa asilimia 0.2. Mwezi Februari 2018 waliuza kwa asilimia 5.5, dhidi ya 5.3% ya Januari 2018.

Ripoti pia imeonesha ukuaji wa soko la kimataifa kwa simu za Xiaomi kwa mwezi Februari, kwa kushika nafasi ya nne nyuma ya Huawei. Soko la Xiaomi liliongezeka hadi 5.1% mwezi Februari 2018 kutoka asilimia 4.8 mwezi Januari 2018.

Oppo ya Uchina imeshika nafasi ya tano kwa upande wa soko la dunia la simu janja, kwa kuuza 3.6% mwezi Februari 2018, kutoka asilimia 3.4 mwezi Januari 2018.

Samsung waendelea kuongoza

Takwimu za mauzo ya kampuni mbalimbali ambapo Samsung imeongoza kwa bidhaa zake kununulika zaidi mpaka kufikia Aprili 2018.

Wakati huohuo, LG imeuza 3.4% kwa mwezi Februari 2018, wakati mauzo ya bidhaa za Lenovo yameshuka kutoka 2.8% Januari 2018 hadi 2.7% mwezi Februari 2018, lakini bado imeendelea kushika nafasi ya saba kwa mwezi wa pili mfululizo katika soko la kimataifa la simu janja.

Motorola nayo imeuza kwa 2.5% mwezi Februari 2018, ikiwa imeshuka kutoka mauzo ya asilimia 2.6 kwa mwezi Januari 2018.

Nokia imekuwa ya mwisho kati ya wazalishaji wa juu katika soko la kimataifa kwa kushuka mauzo yake ya Februari 2018 kulinganisha na ya Januari 2018. Mwezi Februari waliuza kwa asilimia 1.7 wakati Mwezi Januari iliuza kwa asilimia 2 na sehemu yake ya soko kiujumla kufikia asilimia 1.7.

Ushindani ni mkubwa sana na kila leo simu janja mpya inatoka; kuongezeka/kuporomoka kimauzo itategemeana na wateja wamevutiwa kiasi gani na bidhaa zenyewe. Usije ukashangaa zile ambazo zimezoeleka kushika nafasi za juu zikaondolewa, chochote kinawezekana!

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Ondoa vitu kwenye Thumbnails kuongeza nafasi
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.