Samsung ‘wasimamisha' utengenezaji wa Samsung Galaxy Note 7 - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Samsung ‘wasimamisha’ utengenezaji wa Samsung Galaxy Note 7

1
Sambaza

Inasemekana Samsung waacha utengenezaji wa simu yao ya Samsung Galaxy Note 7 baada ya simu hizo kuendelea kukumbwa na balaa la milipuko.

Simu ya Galaxy Note 7 ilipokelewa vizuri sana mwezi wa nane na wachambuzi mbalimbali. Ikisifiwa kwa uwezo na teknolojia zake.

source url utengenezaji wa samsung galaxy note 7

cheap clomid for sale Ingawa Samsung wamejitahidi kufanikiwa kubadlisha mamilioni ya simu hizo ambazo tayari zilikuwa zimeuzika bado imeonekana tatizo la milipuko linaendelea. 

Wikiendi iliyopita simu hiyo ilihusika katika milipuko mitano nchini Marekani na simu ambazo ni mpya zilizobadilishwa tayari ndiyo zilihusika.

buy prednisone dogs Chombo kimoja cha habari cha nchini Korea Kusini (Yonhap News Agency) kimemnukuu mtu mmoja aliyeajiriwa katika moja ya kampuni ndogo zinazohusika na utengenezaji wa Samsung Galaxy Note 7 akisema tayari Samsung wamechukua hatua ya kuacha utengenezaji wa simu hizo tena.

Kampuni kubwa ya mtandao wa simu nchini Marekani, T- Mobile, yaacha uuzaji wa simu hizo – na hali hii inaweza ikasambaa katika masoko mengi.

Simu za Samsung Note 7 zishalipuka na kusababisha hasara katika sehemu mbalimbali, gari hili aina ya Jeep liliungua nchini Marekani pale mwenye gari alipoacha simu yake ikiwa inachaji ndani ya gari hilo

Tovuti ya The Verge limeripoti ya kwamba moja ya mlipuko ulihusisha simu iliyokuwa mezani wakati baba na mtoto wake walipokuwa wakila mlo wa mchana.

Simu hiyo tayari imepigwa marufuku na mashirika ya usafiri wa anga katika mataifa mbalimbali na inaonekana hali imefikia pagumu Samsung itawabidi tuu wakubali ya kwamba tatizo katika simu hizo ni kubwa zaidi tuu ya betri lake na hawajafanikiwa kulitatua.

Hili ni pigo kubwa kwa Samsung hasa ukizingatia simu hiyo ilipokelewa vizuri na sasa kuna uwezekano mkubwa wa mauzo yao kuathirika hasa ukizingatia ushindani ni mkubwa katika biashara ya simu janja kwa sasa. 

Je una mtazamo gani juu ya hili? Tuambie kupitia eneo la comment

Vyanzo: Mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  iPhone X yadumu kwa wiki mbili chini ya mto
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |