Samsung ambao wamekuwa wakifanya vizuri kwenye soko la ushindani bado wameendelea kutoa simu janja na kwa mwaka huu wana rununu ya kwanza ambayo ina kamera tatu nyuma, inaitwa Galaxy A7 2018.
Simu hiyo inaonekana kuwa nzuri na ya kuvutia kwa sababu mbalimbali lakini kubwa ni kuwa na kamera ambazo lenzi yake inatoa picha ambazo ni ang’avu bila kusahau kutokuwa ghali.
Sifa za Galaxy A7 ya mwaka 2018.
Kipengele |
Maelezo |
Kipuri mama/Uwezo wake | Jina la prosesa iliyowekwa huko haijafahamika ingawa kasi yake ni 2.2GHz. |
Kioo | Kioo kina urefu wa inchi 6, rangi za ubora wa hali ya juu (FHD+ Super AMOLED) na kiujumla simu yenyewe ina uzito wa gramu 168. |
Kamera | Upande wa nyuma: Zipo tatu; yenye MP 5, MP 24 na MP 8.
Kwa mbele: Ipo moja tu na ina MP 24. |
RAM/Memori ya ndani | RAM GB 4 au 6 na diski uhifadhi ni GB 64/128 huku ikwa na uwezo wa kuweka memori ya nje mpaka GB 256 |
Betri/Programu endeshi | 3300mAh ndio nguvu ya betri yake ikiwa na Android 8 (Oreo) upande wa programu endeshi. |
Mengineyo | Rangi: Bluu, Nyeusi, Dhahabu na Udhurungi.
Mawasiliano: 4G VoLTE. Pia ina Bluetooth v5.0, ANT+, NFC, GPS, GLONASS, Beidou na sehemu ya kuchomeka spika za masikioni ukubwa wa 3.5mm. |
Galaxy A7 2018 inatazamiwa kuanza kupatikana duniani kote katika siku za usoni na bei ya ughaibuni ni $410|Tsh. 943,000.
Vyanzo: Gadgets 360, Engadget