Hatimaye Apple wameshinda rufani waliyokuwa wamekata dhidi ya Samsung; Apple italipwa $120 milioni kama fidia.
Baada ya mvutano wa huku na kule sasa Apple kulipwa na Samsung kutokana na kuiga vitu mbalimbali kutoka kwenye simu janja zinazotengezwa na Apple (iPhone). Kuigwa huko kunajumuisha jinsi ya kutoa ‘lock’ kwa njia ya kupangusa (slide lock) kwenye simu janja na tableti zinazotengenezwa na Samsung.
Jaji aliyetoa hukumu hiyo alisema kuwa haikuwa sahihi kwa Jaji aliyekataa kutoa hukumu ambayo Apple wangelipwa dola millioni 119.6 (sawa na zaidi ya Tsh 263bn) na kuipeleka kesi hiyo mahakama ya rufaa akitaka kujua kama hukumu kiwango hicho cha pesa kiongezwe au la!
Vitu ambavyo Samsung inadaiwa kuiga ni features kama kufungua lock ya simu kwa njia ya kupangusa, kurekebisha ‘automatically’ namba ya simu ya mtu unayetaka kuwasiliana nae. Maamuzi yakiyotolewa mwezi Feb yaliyadai madai hayo yalikuwa hayana maana.
Kwa kosa la kuiga kurekebisha ‘automatically’namba ya simu ya mtu unayetaka kuwasiliananae tu ilibidi Apple walipwe $98 milioni (zaidi ya Tsh 215bn) milioni ambapo awali kosa hilo lilionekana sio la msingi.
Ingawa na kushinda rufani lakini Apple nao walikuwa matatani katika kesi inayofanana na hii. Soma hapa kujua zaidi kilichoikuta Apple wiki ilyopita. Tupe maoni yako.
Vyanzo: Telegraph, mitandao mbalimbali.