Kampuni ya Samsung yatajwa kuwa yenye thamani zaidi Korea Kusini miaka 7 mfululizo

0
Sambaza

Kampuni ya Samsung Electronics upande wa uzalishaji wa Smartphone (Samsung Electronics Co.’s smartphone brand Galaxy) imetajwa kuwa ndiyo yenye jina (Brand) lenye thamani zaidi Kwa nchi ya Korea Kusini kwa miaka saba mfululizo.

Samsung iliendelea kushika nafasi ya kwanza kupitia ripoti iliyotolewa na Kampuni ya utafiti ya Korea Kusini ya Brandstock. Kampuni hiyo ya Brandstock ilitoa ripoti yenye alama 940.98 kwa kampuni ya Samsung
katika jumla ya alama 1000.

SOMA PIA:  Samsung yaweka rekodi kwa kupata faida ya mamilioni ya dola ndani ya siku moja

Kampuni ya maduka ya uzaaji wa bidhaa mbalimbal ya E-mart wameshika nafasi ya pili, nafasi tatu ilichukuliwa na Kampuni inayojihusisha na mambo ya Intaneti ya Naver na Benki ya Korea Kusini ya KB Kookmin ilishika nafasi ya nne.

airtel tanzania bando

Kampuni ya Samsung yatajwa kuwa yenye thamani zaidi Korea Kusini miaka 7 mfululizo

Kampuni ya Samsung yatajwa kuwa yenye thamani zaidi Korea Kusini miaka 7 mfululizo

Ushindi huu unafatia ule wa Simu yake ya Galaxy S8 na Galaxy S8+ wa kutangazwa kuwa ndio simu bora kwa mwaka 2017 huko Shanghai, China katika mkutano wa mambo ya simu wa Mobile World Congress (MWC 2017).

SOMA PIA:  Nile X: Simu janja ya kwanza kutengenezwa Misri yazinduliwa

Kampuni ya Samsung licha ya kupata msukosuko wa simu yake ya Galaxy Note 7 mwaka jana bado imeendelea kuaminiwa na watu wengi duniani kwa ubora wa bidhaa zake.

Aidha katika hatua nyingine kampuni ya Samsung Galaxy imethibitisha uzinduzi wa simu yake mpya ya Galaxy Note 8 kwamba utafanyika huko Marekani mwezi wa Septemba 26 mwaka huu.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com