Ni jana tuu tumeandika kuhusu taarifa zinazoonesha Samsung wameacha rasmi kutengeneza simu za Samsung Galaxy Note 7.
Simu hizo zimekuwa na majanga ya kulipuka kwa sana na hata pale ambapo kampuni hiyo iliingia hasara kwa kurudisha simu zaidi ya milioni 2 kiwandani na kuzirekebisha kwa kubadili mabetri yake.
Tatizo la simu za Galaxy Note 7 limeonekana ni kubwa zaidi ya ubadilishaji wa betri. Kuna uwezekano mkubwa mfumo mzima wa umeme wa ndani ya simu una makosa.
Sasa ni rasmi, kampuni ya Samsung imewaomba watu wenye simu hizo kuacha kuzitumia mara moja na kuhakikisha zimeisha chaji na kujizima.
Samsung Galaxy Note 7 zilipata sifa ya kuwa simu bora zaidi ya Android pale zilipoingia sokoni mwezi wa nane mwaka huu, ila sasa inaonesha Samsung wanaukubali ukweli ya kwamba toleo hili la simu za Note limekuwa gundu linaloitaji kubaki kwenye historia.
Ni muda mzuri wa huo kujikita zaidi katika toleo la Note 8 na kuona ni jinsi gani waweze kuepusha janga kama hili kutokea tena baadae.
Soma Pia
Vyanzo: WSJ na mitandao mbalimbali
One Comment
Comments are closed.