Samsung yazinduliwa rasmi kwa nchi za Afrika nchini Kenya

0
Sambaza

Samsung S8 ambayo ni simu janja toleo jipya kutoka Samsung baada ya maswahibu ya Samsung Note 7 kulipuka, n.k sasa ni rasmi uzinduzi wa Samsung S8 umefanyika Kenya kuonesha rasmi simu hiyo inapatikana Afrika.

Uzinduzi huo ambao ulihudhuriwa na Mkurugenzi mtendaji Bw. Jung Hyun Park ambaye pia ni Makamu wa rais wa kampuni ya Samsung Eletcronics kwa nchi za Afirka Mashariki. Samsung S8 imekuja kwa nia ya kurudisha uaminifu kwa wateja na wapenzi wa simu za Samsung.

Maandalizi ya uzinduzi huo yalichukua takribani mwezi mmoja huku muda huo ukikuwa ukitumiwa kuwaambia watu wajisajili kwa ajili ya kutaka kufanya manunuzi kabla ya uzinduzi (pre-order) ambapo faida yake ni kupata vitu vya ziada vinavyokuja na simu gharama yake ikiwa karibu Ksh 13,000|Tsh 280,983.85

Watu wakipata maeelezo kuhusu Samsung S8 mwingine akifurahia uwezo wa Samsung S8 huko Kenya.

Sifa za Samsung S8 kwa uchache

Samsung S8 zipo za aina mbili; S8 na S8+. Sifaa kuu zikiwa kamera ya mbele ikiwa na 12MP F1.7, uwezo wa kuhifadhi vitu wa mpaka GB 64 na uwezo kukubali memori kadi ya mpaka GB 256 na kubwa kabisa ikiwa na uwezo wa kungunga kwa kutumia alama ya vidole au kwa jicho.

SOMA PIA:  Uwekezaji wa Nokia kwenye afya na teknolojia ya VR

Soma pia: Uchambuzi wa Samsung S8

Muonekano wa Samsung S8

Bei yake?

Bei ya Samsung S8 ni Ksh 84,999|Tsh 1,838,232.12 na Samsung S8+ ikiuzwa Ksh 94,999|Tsh 2,054,497.27 kwa maduka yote ya Samsung huko nchini Kenya zikipatikana kwa rangi nyeusi, kawahia na dhahabu ambayo haijakolea. Nchini Tanzania utaweza kuzipata kwa bei isiyo mbali sana na hizo tulizozitaja.

Samsung S8 ni kipimo cha kujua kuwa iwapo Samsung kweli makosa yaliyotokea kwenye simu iliyotangulia wamejirekebisha na kama kweli wamedamiria kurudisha uaminifu kwa wapenzi wa simu za Samsung.

Vyanzo: Bunisess Insider, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com