SanDisk imeleta memori kadi ya ukubwa wa GB 400

0
Sambaza

Memori kadi ya GB 400? Ni ukweli, SanDisk imeleta memori kadi ya ukubwa wa GB 400.

Kampuni ya Western Digitial inayomiliki biashara ya memori kadi za SanDisk wametambulisha memori kadi hii mpya ya ujazo wa GB 400 katika onesho la IFA 2017 linaloendelea huko Berlin, Ujerumani.

memori kadi ya ukubwa wa GB 400

Memori kadi ya ukubwa wa GB 400, SanDisk.

Baada ya uzinduzi wake ni muda mfupi inatarajiwa kuingia sokoni kwa kiasi cha Dola za Kimarekani zipatazo 250 (Takribani Tsh 560,000).

SOMA PIA:  Uwezo wa kuhama mtandao wa simu bila ya kubadili laini: Vitu muhimu vya kufahamu

Soma Pia – Jinsi ya Kutambua kama Memori kadi (SD Card) ni feki au la!

airtel tanzania bando

Sifa ya memori kadi hii ni kwamba ina spidi ya UHS-1 yaani inaweza kusafirisha 100MB/s ambapo ni sawa na picha 1,400 kwa dakika moja. Pia inaweza kuhifadhi video ya masaa 40 yenye kiwango cha 1080p.

Memori kadi hii itawasaidia watumiaji Simu Janja na Kamera kuwa na uwezo mzuri kuhifadhi vitu vingi kwa wakati mmoja.

Kwa sasa hii ndio memori kadi yenye ukubwa zaidi kuliko nyingine. Memori kadi iliyokuwa inashikilia rekodi ya ukubwa ni ile iliyotengenezwa na Samsung yenye ujazo wa uhifadhi wa 256GB.

 

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com