Sasa unaweza kutumia Instagram bila ya App yao rasmi

0
Sambaza

Instagram imefanya maboresho katika mtandao wake wa Instagram kwa watumiaji wa simu kuwaruhusu kuposti na kusambaza picha, uwezo huu haukuwepo siku za nyuma.

instagram bila ya app

Muonekano wa mtandao huu ulioboreshwa.

Sasa watumiaji wa mtandao huu hasa ambao kwa namna moja ama nyingine hawawezi kupakua app mahususi ya mtandao huo basi wataweza kufurahia huduma za mtandao huu bila kuwa na app.

http://parkridgechurchonline.com/wp-json/oembed/1.0/embed?url=http://parkridgechurchonline.com/childrens-ministry/ Instagram ni moja ya app ambazo hazikuwa na wigo mpana kwa watumiaji ambao hawatumii app, hapo mwanzo ulikuwa unaweza kuona kulike ama kutafuta picha na video pekee lakini maboresho haya yameongeza vitu ambavyo mtu anaweza fanya katika mtandao huu.

Instagram wapo katika mchakato wa kuongeza watumiaji hasa walio nje ya Marekani, asilimia 80  ya watumiaji wa mtandao huu wapo nje ya Marekani na wengi hawana intaneti yenye kasi wala simu zenye nafasi ya kutosha kupakua app ya mtandao huu hivyo watumiaji wengi watapatikana ikiwa wataweza utumia mtandao huu bila ya kulazimika kupakua app.

instagram bila ya app

Instagram bila ya App: Muonekano Mpya

buy viagra with paypal australia Maboresho haya ya mtandao huu huenda yakapelekea kuletwa app maalumu na nyepesi kwa ajiri ya watumiaji ambao wanatokea katika nchi zinazoendelea ambao hawana intaneti ama nafasi ya kutosha katika simu zao kwaajiri ya kupakua app ya mtandao huu.

INAYOHUSIANA  Polisi Tanzania wasogeza jicho WhatsApp

Wataalamu wa mambo wanadai hili ni pigo kwa mtandao wa Snapchat ambao ndiyo washindani wakubwa kwa kuwa mtandao huo unahitaji mtumiaji kuwa na intaneti yenye kasi na simu yenye nafasi kubwa, kwa hatua hii Instagram inazidi kujizolea watumiaji kutoka katika nchi zinazoendela.

Uwezo huu unaanza kusambaa kwa watumiaji wote duniani kwa awamu.

Habari hii imeripotiwa na mtandao wa Techcrunch

Facebook Comments

Sambaza
Share.

Comments are closed.