Satelaiti ya Facebook ya kufikisha intaneti kasi Afrika yalipuka

Satelaiti ya Facebook ya kufikisha Intaneti ya kasi Afrika yalipuka

0
Sambaza

Facebook wapata janga katika juhudi zao za kusambaza intaneti baada ya satelaiti ambayo Facebook ingeitumia kwa mawasiliano ya intaneti yenye kasi barani Afrika kuharibiwa.

http://countryqwips.com/product-category/music/?orderby=date

Satelaiti hiyo iliharibiwa katika mlipuko uliotokea eneo la Cape Canaveral jimbo la Florida, Marekani siku ya Alhamisi.

Satelaiti hiyo kwa jina Amos-Six ilikuwa imebebwa na roketi ya Falcon Nine ambayo ililipuka ilipokuwa ikifanyiwa majaribio ya kujiandaa kwa safari ya siku ya Jumamosi.

Mlipuko huo ulitokea wakati roketi hiyo ilikuwa ikijazwa mafuta na kutikiza majengo yaliyokuwa umbali wa kilomita kadha.

Satelaiti ya Amos-6 inakadiriwa kuwa na thamani ya $200m|Tsh bil. 440 na ilimilikiwa na kampuni kwa jina ‘Spacecom’.

Amos 6 xplosion

http://artguildmf.org/bank-offers-new-display-opportunity/ Moshi ulitokana na mlipuko wa satelaiti iliyoitwa Amos 6 ya Falcon 9.

Hakuna aliyejeruhiwa katika mlipuko huo. Facebook wanasema kuwa wataendea kujitolea wakiwa na lengo la  kufikisha huduma ya mtandao kwa kila mtu na kufanya bidii hadi kila mtu apate nafasi na manufaa ambayo yangetokana na satelaiti hii.

Vyanzo: BBC, Space news

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  Facebook yalegeza masharti kuhusu matangazo ya sarafu za kidijitali
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.