Sayari 7 mpya zilizo sawa na dunia zagundulika! #Utafiti - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Sayari 7 mpya zilizo sawa na dunia zagundulika! #Utafiti

1
Sambaza

Kwa wale watu ambao bila utafiti basi cheo chao hakiwezi kukubalika wanaofahamika kama Wanasayansi, na mwaka huu wamekuja na jambo jingine jipya kabisa!

Sayari mpya 7 zilzogunduliwa hivi karibuni.

Wataalamu wa masuala ya anga za juu wa Marekani wakishirikiana na wengine duniani, wamefanya ugunduzi mkubwa wa go site sayari saba zenye ukubwa sawa na wa Dunia ambazo zinaizunguka nyota mojawapo kama ilivyo kwa dunia kulizunguka Jua.

http://gaethicswatchdogs.org/category/in-the-news/ Wanasayansi hao wa anga za mbali kutoka Marekani, Uingereza na Ubelgiji, wamebainisha kuwa sayari hizo saba walizozigundua zinaizunguka nyota ijulikanayo kwa jina la Trappist One.

Wanasayansi wanaamini kwamba takribani katika kila nyota moja kuna uwezekano wa kuwepo sayari moja ingawa wanasayansi hao wamesisitiza kuwa kwa teknolojia iliyopo sasa inaweza kuwachukua maelfu ya miaka kuzifikia sayari hizo.

>Mengineyo kuhusu sayari 7 mpya.

  • Sayari tatu kati ya hizo saba zilizogundiliwa zipo karibu na nyota hiyo (Trappist One) na zina sifa tofauti.
  • Inaonyesha kuwa sayari hizi tatu kati ya hizo saba zilizogunduliwa zipo katika ukanda unaoweza kuruhusu viumbe kuishi, kwani maji yanaweza kupatikana na maisha ya viumbe hai yanaweza kuendelea, cha kushangaza zaidi ni kwamba http://wallacespuds.com/uncategorized/gallery-post-format/ maisha yanaweza kuwepo hata katika uso wa sayari hizo.
INAYOHUSIANA  Ijue ndege ya Boeing 787-8 Dreamliner

Kuzifikia Sayari hizo ni changamoto sana na hata kwa mwendokasi wa mwanga unaosafiri kwa kasi sana inaweza ikawachukua miaka 40 kwa wanasayansi kuzifikia sayari hizo na swali wanalojiuliza sasa ni katika anga hilo kuna nini?

Ugunduzi huu unatajwa na wanasayansi hawa kuwa ni mafanikio makubwa na umewaingiza katika ukurasa mwingine na kubakiwa na swali moja tu kwamba ni lini watazifikia sayari hizo?

Chanzo: BBC

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|