Screenshot ndio habari ya mjini sidhani kama kuna mwenye simu janja ambae hajui kufanya hivyo. Ni njia rahisi sana ya kufikisha ujumbe kama ulivyo kwa mlengwa, maana kila kitu kinakuwa hakijatiwa chumvi hata kidogo
Sawa ni njia rahisi lakini je, huwa unafanikiwa kupiga ‘screenshot’ hiyo kwa urahisi kabisa au ndio mpaka ubonyeze vibonyezo vingi kwa wakati mmoja?
kama jibu ni ndio basi njia hii itakua ndio mkombozi wako wa dhati kwa swala hilo. Kama kawaida leo TeknoKona inakuletea maujanja mengine
JINSI
kwanza kabisa ingia katika soko la Google Play Store na kisha pakua App ya Screenshot Assistant
Baada ya kuishusha ukiifungua tuu kwa mara ya kwanza itakua inakupa maelezo kadhaa juu ya jinsi ya kuitumia. Baada ya hapo itakubidi ufanye maboresho kudogo kwa kuchakua App ambayo itakua katika mstari wa mbele katika kukupa msaada
Ukichagua Screenshot assistant kama kama App ya msaada (assistant) hutakua na uwezo wa kutumia Google Now kama App yako ya msaada kama ilivyokua mwanzo. ukimaliza uchaguzi huo kisha ‘Save’
Jinsi ya kupiga Screenshot’ ni rahisi sana kwani itakubidi ubonyezo kibonyezo cha ‘home’ (cha kurudia katika uso wa simu) kwa sekunde chache bila kuacha na kisha itajipiga
Kizuri kuhusiana na App hii ni kwamba ukishapiga hiyo Screen shot’ utapata machaguzi mengine kabambe kama vile ku’crop’ hiyo screenshot’ na mambo mengine mengi kama vile ku’share.
Baada ya hapo unaweza ukasave na ukaanza kuitumia wewe mwenyewe binafsi au ukawatumia watu uliokusudia (hah!).
Android; Screenshot Assistant
Hii ni App nzuri tena kama unataka App ya kupiga Screenshot’ kwa urahisi kabisa…… hii ndio yenyewe