Shirika la ndege la Uingereza lakumbwa na tatizo la kompyuta.

0
Sambaza

Shirika la ndege la Uingereza limekumbwa na msukosuko baada ya kupatwa na tatizo la kompyuta katika viwanja viwili vya ndege vikubwa jijini London.

shirika

Mizigo ikiwa imejaa katika uwanja wa ndege baada ya mfumo wa kompyuta kupata matatizo.

Shirika la ndege la Uingereza limethibitisha kwamba tatizo hilo sio kwa sababu ya udukuzi ama makosa ya kimtandao bali linatokana na kushindwa kufanya kazi kwa kifaa.

Tatizo hili limedhuru mtandao wa kampuni hiyo, app yake ya simu na pia vituo vyote vya simu vya kampuni hiyo. Kimsingi hakuna ndege iliyoweza kutua ama kuruka katika viwanja hivyo viwili kwa kuwa mtandao wa kukagua mizigo na kuwakagua abiria haufanyi kazi kufuatia tatizo hili.

SOMA PIA:  Teknolojia ya FaceID kuruhusu uso mmoja tu kusajiliwa

Tukio hili limepelekea Shirika hilo la ndege kusitisha zaidi ya safari 1000 za ndege kwenda sehemu mbalimbali duniani siku ya jumamosi. Hatahivyo wataalamu wa usafiri wa anga wanadai kwamba itachukua siku tatu mpaka nne kwa shirika la ndege Uingereza kufanikiwa kurudisha hali ya kawaida.

Lawama mwisho wa siku zinarudi kwa shirika la ndege Uingereza kwa kutokuwa na mpango mbadala madhubuti ambao ungeweza kusaidia katika kipindi hiki ambacho mfumo wa mtandao haufanyi kazi. inategemewa kwamba tukio hili litafanya mashirika ya ndege kufikiria njia mbadala za kuendesha shughuli zake pindi njia za kawaida zitakaposhindwa.

SOMA PIA:  Teknolojia ya FaceID kwenye iPhone X 'yamvuruga' John Cena

shirika la ndege la uingereza

Wakati makala hii inachapishwa tayari tatizo hili limetatuliwa na shughuri zimerudi katika viwanja hivyo viwili huko London.

Endelea kufuatilia mtandao wako wa Teknokona kwa habari motomoto za Teknolojia, pia tufuate katika mitandao ya jamiii kama Facebook Twitter na Instagram.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com