Shiriki Olimpiki ndogo iliyoanzishwa na Google! #Gemu

0
Sambaza

Wakati pazia la michezo ya olimpiki likiwa linafunguliwa huko katika jiji la Rio Brazil Google nao hawako mbali baada ya kuleta magemu ya michezo mbalimbali ya olimpiki katika app yake ya Google.

Google-doodle olimpiki

Magemu hayo ambayo yamekuja katika ubunifu wa matunda aina mbalimbali yatakuwepo kuchezwa mpaka tarehe 21 mwezi huu ni pamoja na Riadha Tennis Mbio za baisikeli kuogelea na michezo mingine mingi ya olimpiki.

Kucheza michezo hii mchezaji itabidi kwanza uwe na app ya GOOGLE na kisha ukifunga utaona Doodle ambayo ukiifungua utakutana na michezo mbali mbali ambayo pia inamaelekezo ya jinsi ya kuicheza.

SOMA PIA:  Alama za vidole kimeo katika simu za Pixel 2 baada ya kusasisha Android 8.1

maxresdefault (3) olimpiki

Pengine hii inaweza kuwa ni chachu ya kuchochea aina hii ya magemu ambayo ni mepesi lakini yanachangamoto na pia hayahitaji vifaa ambavyo ni vya kipekee. Miaka ya karibuni tumeona mfumo wa magemu mepesi kuchezwa yakipata mafanikio katika soko Angry bird ni mfano mzuri wa magemu mepesi ambayo yaliweza kuteka soko.

Facebook kupitia app yake ya Messenger tayari wamekwisha anza kutumia magemu rahisi kuvutia watumiaji hivyo haitakuwa jambo la ajabu mitandao mingine ikiiga swala hili.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com