Shusha Video Za Youtube Kwa Kutumia VLC! - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Shusha Video Za Youtube Kwa Kutumia VLC!

0
Sambaza

Mara nyingi huwa tunaburudika wakati tunaangalia video katika mtandao wa Youtube. Video zingine zinatupendeza sana kiasi cha kwamba tunatamani kuziangalia mara kwa mara.

Video Za Youtube Kwa Kutumia VLC

Video Za Youtube Kwa Kutumia VLC

Ili tuwe nazo karibu inabidi kuzishusha katika vifaa vyetu, hapo sasa ndipo linapokuja tatizo. Jinsi ya kushusha video hizo, sawa kuna njia nyingi za kushusha video hizo, lakini ni ipi rahisi?

Leo TeknoKona itafanya juu chini kwa kuhakikisha kuwa inakutoa tongo tongo. Yaani mpaka ukimaliza kusoma makala hii utakuwa ni mtaalamu kwa kushusha video za youtube mpaka kwenye kifaa chako kwa urahisi kabisa

http://familymedspa.net/blog/ Ili Kujua Ujanja Huu Fuatilia Njia Hizi!

INAYOHUSIANA  VLC haipatikani kwa baadhi ya simu za Huawei

1. Fungua Youtube na nenda katika video unayoipenda. Nakili link (URL) ya video hiyo

2. Fungua VLC na kisha nenda katika Media > Open Network Stream. Bofya Ctrl + V.

Video Za Youtube Kwa Kutumia VLC
follow Ile link uliyoinakili inajiweka (paste) katika kiboksi chini ya neno Network  Protocol. Baada ya hapo bonyeza katika kibonyezo cha Play

3. Hapo utaona video yako ikicheza katika VLC lakini bado utakua haujaishusha

4. Nenda katika http://islam101.ca/places/canada/alberta/edmonton/medical/millbourne-mall-medical-center/ Tools > Codec Information. Kwa chini kuna kiboksi chenye neno Location pembeni yake. “Right Click” kiboksi hicho na kisha chagua Select All baada ya hapo bonyeza Ctrl + C


5. Fungua kivinjari na kisha bofya Ctrl + V ili kuweka nakala katika sehemu ya kuingia katika mtandao kisha bofya Enter

INAYOHUSIANA  Youtube: Kipengele cha Dark Mode kwenye simu

6. Video yako itaanza kucheza katika kivinjari. Hapo unaweza uka ‘Right Click’ na ukachagua ‘Save Video As’. Unaweza andika jina la video kama unavyotaka. Bonyeza neno Save na kisha video yako itaanza kujipakua katika kompyuta yako

Mpaka kufikia hapo, nikupe hongera kwani na wewe bila shaka umeshakuwa mtaalamu wa kushusha video za Youtube kwa kutumia VLC katika kompyuta yako. Kama umekwama kwa namna yeyote, naomba uniandikie hapo chini sehemu ya comment ili niweze kukusaidia

Soma Pia – Njia za kupata data zako zilizopotea/kufutwa ktk simu/tableti ya android

Pia kama ungependa TeknoKona iandike kuhusu jambo Fulani ili wote tufanikiwe ingekuwa vizuri ukiniandikia lako la moyoni hapo chini sehemu ya comment

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Comments are closed.