Sigara ya kielektroniki yalipuka mfukoni mwa mtumiaji na kumuunguza

Sigara ya kielektroniki (E-Cigarette) yalipuka mfukoni mwa mtumiaji na kumuunguza

0
Sambaza

Watumiaji wa sigara za elektroniki, yaani E-cigarettes, wanazitumia kwa sababu zinasifika ya kwamba ni salama zaidi dhidi ya magonjwa ya saratani (cancer) ukilinganisha na sigara za kawaida…ila inaonekana zinaweza kukudhuru kwa njia zingine pia.

E Cigarette sigara ya kielektroniki

Sigara ya kielektroniki

Mwanaume mmoja Marekani anaweza kufanya maamuzi ya kutokutumia tena sigara za kielektroniki baada ya kuumia kutokana na mlipuko wa sigara ya hiyo (e-cigarette) iliyokuwa mfukoni mwake.

Tukio hilo lilitokea akiwa kazini na wenzake katika duka kubwa la uuzaji divai (Wine) jijini New York huko nchini Marekani.

sigara ya umeme e cigarette kulipuka

Muonekano wakati sigara hiyo ikilupukia mfukoni mwa Bwana Gooding

sigara ya umeme

Hali ya Bwana Gooding. Kaungua eneo la paja na mkono.

Video za usalama za dukani humo zilifanikiwa kurekodi tukio zima la mlipuko huo. Video hizo zimeonesha Bwana Gooding, mwenye umri wa miaka 31 akipiga stori na wafanyakazi wenzake pamoja na mteja mmoja aliyekuwa anajiandaa kuondoka – ghafla mlipuko wa sigara hiyo ulisababisha watu kutawanyika kwa hofu huku wakimuacha Bwana Gooding akihangaika kuitoa sigara hiyo iliyokuwa ikiwaka na kulipuka kutoka mfukoni mwa suruali yake.

INAYOHUSIANA  Aina tatu tofauti za vimemeshi vyenye uwezo wa juu

here Tazama video hii inayoonesha jinsi jambo hilo lilivyotokea;

http://maxwell3d.net/2012/03/terrain-textures-at-ubisoft/ Mwanasheria wake amesema Bwana Gooding ameungua eneo kubwa la kwenye paja na kuna uwezekano akaitaji kufanyika upasuaji (surgery) kama sehemu ya matibabu.

Hadi sasa inaaminika mlipuko huo ulisababishwa na mfumo wa betri wa sigara hiyo.

Hii si mara ya kwanza kwa sigara za mfumo wa umeme kulipuka, na tayari wateja kadhaa wameshafungua kesi za madai dhidi ya makampuni kadhaa ya utengenezaji wa sigara hizi. Kwa kiasi kikubwa kuna uwezekano mkubwa Bwana Gooding naye akafungua mashitaka dhidi ya kampuni iliyotengeneza sigara iliyomlipukia.

where can i buy Prozac Soma Pia – Sigara za Umeme, E-Cigarettes, zinasaidia watumiaji kuacha kuvuta sigara

INAYOHUSIANA  Betri la Samsung Galaxy Note 9 ni salama

Una mtazamo gani na sigara hizi za kielektroniki?

Kumbuka kusambaza makala na pia kuungana nasi kupitia Facebook, Twitter, Instagram, YouTubeTelegram na Google Plus

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.