SIGNAL: Facebook Waja Na Kipengele Kipya Kinachosaidia Waandishi Wa Habari!

0
Sambaza

Facebook kwa sasa inaongoza katika mitandao ya kijamiii yenye huduma nyingi hii ni ukiachana na huduma zile za kawaida zilizo zoeleka kama kutuma na kupokea ujume na kupiga simu.

Facebook imezindua kipengele kingine rasmi kwa ajili ya waandishi wa habari (signal). Hii ikiwa msaada kwao juu ya kujikusanyia habari na matukio mbali mbali duniani

Kitu hiki kimefananishwa na kile cha twitter kinachoitwa ‘Trends’ ikiwa na maana ya ‘Mwenendo’. Unaweza ukadhani kipengele hiki ni cha Facebook peke yake lakini kinafanya kazi mpaka katika mtandao wa kijamii wa instragram unaohusisha picha na video.

Kipengele Cha 'Signal'

Kipengele Cha ‘Signal’

Kipengele hiki kitasaidia waandishi wa habari kuvuna habari kupitia mitandao ya kijamii ya Facebook na instragam. Hebu fikiria ni matukio mangapi yanayotokea mtaani na raia wanakuwa wakwanza kuyaweka mtandaoni? jibu unalo! waandishi wa habari wanaweza tumia mitandao ya kijamii hiyo (facebook na instagram) ili kupata taarifa (habari) hizo

SOMA PIA:  Maboresho: Instagram Direct yazidi kunogeshwa .

Signal pia ina vipengele vipya ambavyo havijawahi kutumika kama vile kile cha ‘Leaderboards’, ukurasa unaosaka na kuchambua data za mazungumzo katika maelfu ya kurasa, ambazo zinaweza kutumia kupima uhalisia wa yale yaliyoandikwa na majina makubwa kama vile wanamuziki na wanasiasa

'Leaderboard'

‘Leaderboards

Dashboard pia linatumika kumrusu mwandishi kuhifadhi picha na post zilizopatikana kutoka Facebook na Instagram na kuziweka katika sehemu ya mkusanyiko (Collections)   ambapo baadae mwandishi anaweza aka ‘click’ mara moja ili kupata uwezo wa kupachika makusanyiko hayo yote katika sehemu (post) moja.

SOMA PIA:  Utafiti: Hizi ndio Apps zinazokula sana Chaji ya Betri na nafasi katika simu za Android

Hii ni njia mojawapo ya njia ya kuwasaidia waandishi wa habari ili kupata taarifa na matukio yenye ukweli juu yake. kama wewe ni muandishi wa habari na untaka kupata huduma hii kuna fomu ya kujaza hapa

Signal itakua ndio chimbuko la ujumbe wa maneno, picha, video na data zingine kupitia Facebook na Instagram na mpaka sasa inatumiwa na waandishi wa habari tuu ambao itawabidi wajaze fomu ya maombi hapo juu ili kukipata kipengele hiki. Kama wewe ni muandishi wa habari hii si ya kukosa. Tuandikie sehemu ya comment kipengele hiki umekipokea vipi pia usiache kutembelea mtandao wako pendwa wa TeknoKonaDotCom. TeknoKona Tupo Nawe Katika Teknolojia.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Mhariri Wa Teknokona Na Mmoja Kati Ya Wafuasi Wa Teknolojia! Tuikuze TeknoKona Wote Basi. Ningependa Kusikia Kutoka Kwako Nitumie Barua Pepe hash@teknokona.com

Leave A Reply

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com