Simu janja 6 za Xiaomi kutopata masasisho tena - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Simu janja 6 za Xiaomi kutopata masasisho tena

0
Sambaza

Simu janja kutoka Xiaomi zimekuwa zikishika kasi kwa maana ya kwamba zinanunuliwa kwa wingi na hivyo kuleta ushindani wa aina yake kwa makampuni kama Apple, Samsung. Masasisho kwenye vitu vya kiteknolojia ni muhimu sana ingawa mambo ni tofauti kidogo.

go to link Hata kama hauna simu janja yoyote kutoka Xiaomi lakini kama ni mfuatiliaji wa makala zetu mbalimbali juu ya uchambuzi wa http://cmminspections.com/cmm-manager-programming/ simu janja mbalimbali za Xiaomi utakuwa unajua kuwa simu hizo moja ya sifa zake ni kuja na MIUI (ipo kwenye simu janja/tabiti za Xiaomi).

Simu janja 6 ambazo hazitopata tena masasisho ni Mi 2/2S, Mi 4i, Redmi Note 4G, Redmi 2, Redmi 2 Prime, na Mi Note ambapo masasisho ya mwisho kwa simu janja tajwa itakuwa ni MIUI  Beta ROM 7.11.16. Sababu ya kuachana na kuendelea kutoa masasisho kwenye simu janja hizo umwzingatia http://laborlawyerkc.com/definition-of-retaliation/ mwaka uliotolewa simu husika, watu ambao bado wanatumia simu hizo, uwezo wa simu janja.

xiaomi

Bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Xiaomi yenye makao yake makuu huko Beijing.

Xiaomi imetoa MIUI 9 kama toleo la majaribio lakini ambalo halitahusisha simu janja ambazo zimeorodheshwa kuacha kupokea masasisho yoyote kutoka Xiaomi.

Kuna wakati inafikia lazima tukubaliane na mabadiliko kutokana na sababu mbalimbali hasa katika ulimwengu wa teknolojia ambao kila siku unakuja na kitu kipya. Masasisho ya mwisho kwenye simu hizo yataanza kupatikana kuanzia mwezi Desemba mpaka Januari 2018.

Vyanzo: Gadgets 360, India Express

Facebook Comments

Sambaza
INAYOHUSIANA  VIdeo za makundi kwenye Instagram sasa ni rasmi
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.