Simu Janja binafsi kupigwa marufuku kwa wafanyakazi wa White House

0
Sambaza

Ikulu ya Marekani, White House inafikiria kupiga marufuku wafanyakazi wake kutumia simu janja binafsi wakati wa kazi kutokana na wasiwasi wa kudukuliwa kwa mawasiliano katika Ikulu hiyo.

Taarifa zinasema kumekuwa na simu janja nyingi binafsi za wafanyakazi wa Ikulu hiyo ambazo zinaonekana kuungwa kwenye mitandao kupitia Wi-fi ya West Wing iliyopo ndani ya White House. Mkuu wa White House John Kelly ambaye simu yake iliathiriwa na wadukuzi mapema mwaka huu binafsi yupo mstari wa mbele kupitishwa kwa marufuku hiyo.

Ikulu ya Marekani:Tahadhali za usalama zimeanza kuchukuliwa kwa kuzuia mtu kuingia na simu katika kumbi za mikutano ya ikulu ambapo kumekuwa na uvujaji wa taarifa kupitia simu.

Simu janja zilizotolewa na White House kwa wafanyakazi wake haziwezi kutuma ujumbe wa maandishi hivyo kuzuia malalamiko ya wafanyakazi hao kushindwa kuwasiliana na na familia zao pindi wanapohitaji kufanya hivyo kwa njia ya ujumbe mfupi.

Aidha, kompyuta zinazotumiwa na wafanyakazi wa ikulu ya Marekani zimezuiwa uwezo wa kutuma ujumbe kupitia Gmail, Google Hangout na baadhi ya tovuti fulani kushindwa kufunguka hivyo kuwalazimu kutumia simu zao binafsi.

SOMA PIA:  Nokia 6: Kuingia madukani mwezi Julai

Wakati wa ziara ya rais Trump nchini China wafanyakazi wa ikulu walioambatana na Rais walizuiwa kutumia simu zao za kawaida kwa wasiwasi wa kudukuliwa mawasiliano yao wakiwa huko.

Hatua rasmi ya upigaji marufuku bado kwa kuwa kumekuwa na mjadala wa pande mbili za wale wanaotaka na wasiotaka marufuku hiyo. Rais Donald Trump amelalamika mara kwa mara juu ya uvujaji wa taarifa za Ikulu kwa vyombo vya habari tangu kuchukua ofisi.

SOMA PIA:  Samsung Galaxy S8: Samsung watengeneza simu rahisi zaidi kuvunjika kisha waitengenezea kikava

Hata hivyo malalamiko hayo ya rais Trump hayaunganishwi na nia ya marufuku inayokusudiwa kwa kuwa wasiwasi mkubwa ni kudukuliwa kwa taarifa muhimu za Ikulu.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni mpenzi na mfuatiliaji wa mambo ya Sayansi na Teknolojia.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com