Simu janja mpya kutoka kwa Google zina matatizo ya kiufundi

0
Sambaza

Hivi karibuni Google imepata sifa lukuki kutokana na simu zake mpya ambazo ni muendelezo wa toleo la kutoka familia ya Pixel ambazo zinatengenezwa na moja ya kampuni nguli kabisa kwenye masuala ya teknolojia hata kuwa ‘ubongo’ wa karibu dunia nzima 😆 😆 😆 .

Ni zaidi ya mwezi sasa tangu simu janja Pixel 2 na Pixel 2 XL kuzinduliwa lakini karibu wateja 100 walionunua simu hizo wamelalamika kutofurahia simu hizo zenye matatizo mawili ya kiufundi na ni wazi kwamba ule usemi wa ‘Adui yako mwombee njaa’ basi unaweza kutumika hapa kutokana na wapinzani wakubwa wa Google kwenye biashara ya simu janja ni Apple na Samsung.

SOMA PIA:  China yawasha mtambo wa umeme wa nguvu za jua unaoelea ziwani

Matatizo yaliyobainishwa ni kwenye upande wa sauti ya juu sana wakati wa kuongea na simu pamoja na tatizo la kujiweka weka alama ya vema pale unaondoa ulinzi kwenye simu hizo (Pixel 2 na Pixel 2 XL).

Simu janaja ya Pixel 2 XL.

Kasoro hizo zilizobanika kwenye simu hizo zinaweza zikapelekea mauzo ya simu hizo kushuka kutokana tu zina matatizo ambalo mojawapo la matatizo yaliyobainishwa unaweza kusitisha kwa kuzima kipengele cha NFC (kipengele hiki kipo kwenye simu za Pixel 2 na Pixel XL) na tatizo la kutoa sauti ya juu linatokea wakati wa kuongea na simu tu.

SOMA PIA:  Mwaka 2017 ulikuwa mwaka salama zaidi kwa safari za anga

Google haijasema mengi kuhusiana na tatizo hilo ingawa imesema tayari timu ya ke inashughulikia matatizo hayo na kutaarifu umma kuwa kwa yeyote aliyenununua simu janja ya Pixel 2/Pixel 2 XL atoe taarifa ili Google watume mafundi wake waje kulishughulikia tatizo husika.

Vyanzo: Engadegt, mitandao mbalimbali

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com