Katika hali ya kuendelea kujidhatiti katika suala zima la biashara ya simu janja LG wamekuja na nyingine ya kuvutia na yenye mashiko kwa wapenzi wa simu janja na katika ulimwengu huu wa sasa ambao unakwenda na teknolojia.
Siku chache zilizopita LG wametambulisha simu janja aina ya LG G6. Simu iliyotangulia kabla ya LG G6 lilikuwa toleo la G5 ambalo halikufanya vizuri na LG wakarudi nyuma na kutathimini vile vyote ambavyo havikupendwa na wanunuaji wa LG G5 na sasa wamekuja na simu nyingine ambayo ni muendelezo wa simu za LG zilizo katika kizazi cha ‘G’.
Sifa za LG G6
- Kioo (display): Kioo kina ukubwa wa inchi 5.7” Quad HD huku ikitumia teknolojia za kuonyesha picha katika ubora wa kisasa.
- Processor: Snapdragon 821 quad-core
- Betri: Uwezo wake ni 3,300mAh
- Kamera: Ina kamera mbili za Megapixel 13 mbele na MP 5 kwa kamera ya nyuma (selfie)
- RAM: GB 4 (ni wazi kwamba kwa ujazo huo wa RAM simu hii haikuwa ikikwamakwama wakati unapoitumia)
- Ujazo: GB 32 wa ujazo wa ndani lakini inakubali memory kadi ya mpaka ujazo wa TB 2
- Programu endeshaji: Inatumia Android 7.0 Nougat ambayo ni toleo la kisasa zaidi la programu endeshaji ya Android
- USB: USB type-C. Ni teknolojia ya kisasa kabisa ambayo inatumika katika simu/kompyuta za matoleo ya hivi karibuni
Simu hii aina ya LG G6 haingii maji lakini pia inaweza kuchajiwa kwa kutumia teknolojia ya bila kutumia USB kuchaji simu bali wa kutumia teknolojia ya wireless. Pia betri yake haiwezi kutolewa (imeunganishwa ndani kwa ndani).
Simu hii inauzwa karibu dola 800 za Marekani (zaidi Tsh 1,760,000) na kwa kuanzia zimeanza kuuzwa huko Austria.
Je, umevutiwa na nini katika LG G6?
Vyanzo: Gizmodo, BBC