Simu milioni 900 za Android hatarini kudukuliwa

0
Sambaza

Utafiti unaonesha takribani simu janja milioni 900 zinazotumia Android na zikiwa na teknolojia ya chip kutoka kampuni ya Qualcomm zipo hatarini dhidi ya udukuzi.

Watafiti kutoka kundi la utafiti wa kiusalama la CheckPoint, wamegundua makosa ya kiusalama yanayoweza wezesha wadukuzi kudukua kwa urahisi simu nyingi sana zinazotumia Android na huku zikiwa na chip za Qualcomm.

Kivipi?

Inasemekana kama mtu akipakua app isiyo salama baada ya kudanganywa na wadukuzi – wadukuzi hao watapata nguvu ya kupata data mbalimbali kuhusiana na simu husika.

Aina ya simu zilizoathirika

  • BlackBerry Priv na Dtek50
  • Blackphone 1 na Blackphone 2
  • Google Nexus 5X, Nexus 6 na Nexus 6P
  • HTC One, HTC M9 na HTC 10
  • LG G4, LG G5, na LG V10
  • New Moto X ya Motorola
  • OnePlus One, OnePlus 2 na OnePlus 3
  • Samsung Galaxy S7 na Samsung S7 Edge
  • Sony Xperia Z Ultra

Hakuna ushahidi kuwa tayari simu hizo zimeathirika ila ukweli ni kwamba mtu yeyote mwenye ufundi na nguvu kubwa katika udukuzi inasemekana anaweza akafanikiwa kuingilia simu hizo. Chip za kampuni ya Qualcomm zinazodaiwa kuja na matatizo katika ‘drivers’ zake za Android inasemekana zipo katika takribani simu milioni 900. Hilo linamaanisha kuwa simu milioni 900 zipo katika hatari kubwa ya kudhibitiwa na wadukuzi.

Simu mbalimbali zinazotumia Android.

Simu mbalimbali zinazotumia Android.

Upungufu unamwezesha mtu wa tatu kumpokonya mmiliki wa simu udhibiti kwani anaweza hata akabadilisha nywila (password) bila yako wewe kujua. Njia moja ya kuimarisha usalama wa simu ni kupata apps kutoka kwa soko maalum la Google Play.

SOMA PIA:  Google kuacha kutoa masasisho kwenye simu janja mbili!

Ila inasemekana tayari kuna simu ambazo zishapata masasisho (updates) yanayoongeza usalama na hivyo kuweka salama simu hizo. Na pia Google na Qualcomm wamesema tayari kuna masasisho mengine yanakuja kwa ajili ya simu nyingi zaidi.

Vyanzo: The Times of India, BBC

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com