Simu mpya ya Google Pixel 2 XL yaingia dosari katika kioo

0
Sambaza

Simu mpya ya Google iliyozinduliwa hivi karibuni imeingia dosari baada ya kugundulika kuwa na shida katika kioo chake, simu hiyo ya Pixel 2 XL ambayo imezinduliwa mwezi huu  mwanzoni ilipata kupigiwa chapuo na mitandao mingi iliyoichunguza.

Imegundulika kwamba kioo cha Pixel 2 XL kimekuwa kinaacha alama za picha zilizopita, yaani ingawa umeshafungua picha ama kurasa nyingine kioo hicho bado kinakuwa na chembechembe ama mabaki ya picha au kurasa iliyopita.

Tatizo hili la kioo kwa kingeleza linajulika kama screen burn-in na halina madhara makubwa kwa utendaji wa kazi wa simu hii ila ni jambo la aibu kwa Google kuuza simu mamilioni ya pesa kisha simu hiyo ikawa na tatizo hata kama ni dogo.

Simu mpya ya Google Pixel 2 XL yaingia dosari katika kioo

Simu mpya ya Google Pixel 2 XL yaingia dosari katika kioo: Tatizo la mabaki ya picha kwa kile ambacho umetoka kukiangalia kwenye simu janja ya Pixel 2 XL.

Hata hivyo tatizo hili limeripotiwa  kwa simu hiyo ya Pixel 2 XL pekee na sio kwa simu pacha ya Pixel 2 ambayo ni ndogo na pia inatumia kioo cha OLED kilichotengenezwa na Samsung wakati Pixel 2 XL yenyewe inatumia kioo cha OLED ila kilichotengenezwa na LG.

Ingawa ubovu huu wa kioo hauwezi kufananishwa na tukio la simu za Samsung kulipuka betri lakini ni wazi kwamba kampuni ya Google imepata pigo kubwa kwa sababu shida hii ya kioo itaharibu uhusiano wa kampuni hiyo na wateja wa vifaa vyake ambavyo ndio kwanza wameanza kutengeneza. Tazama picha mnato kujua zaidi.

SOMA PIA:  Google yazuia watu kusema ya moyoni

Ingawa Google wamesema wanachunguza juu ya madai ya dosari hizo katika kioo, lakini ni wazi kwamba tayari mambo yamekwisha haribika kwani mitandao mingi imeripoti dosari hizi.

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com