Baada ya uvujaji na taarifa nyingi hatimaye simu kutoka kampuni ya Uchina ya Oppo Find X imezinduliwa jana Paris nchini Ufaransa.
Simu hiyo inatarajiwa kuanza kuuzwa mwezi Agosti mwaka huu na haijajulikana kama itapatikana katika masoko yote duniani au itaanza Uchina kisha kufuatiana mengine. Kwa kawaida Oppo imekuwa ikilenga masoko ya Uchina, India, Ufilipino na baadhi ya nchi za Asia.
Oppo Find X inakuja na teknolojia ya kamera ya mbele yenye kujifunga na kujifungua kitu ambacho kitawavutia watumiaji wake wengi. Kamera hiyo itajifungua tu pale mtumiaji atakapotaka kuitumia kwa picha za selfie.
Ikiwa na prosesa bora na ya kisasa ya Snapdragon 845 kadhalika katika upande wa uhifadhi wa ndani nako kuna mapinduzi makubwa; 256GB ambapo kwa ukubwa huo hakuna ulazima wa kutumia au kuongeza memori ya ziada ndani ya simu yako.
Kama utapenda kuongeza memori kwenye simu hiyo pia waweza kuweka yenye ukubwa mpaka wa 400GB. Kwa upande wa RAM ina ukubwa wa 8GB pamoja na mfumo endeshi wa Android 8.1 Oreo.
Oppo Find X inakuja na kioo kikubwa cha inch 6.42 chenye teknolojia ya AMOELED chenye uwezo wa kuonesha rangi milioni 16.
Aina ya Betri ni Li-Ion na ukubwa wake ni ujazo wa 3730mAh yenye mfumo wa kutotoka kwenye simu (Non-removable).
Sifa za Oppo Find X
Aina ya kioo: AMOLED
Ukubwa wa kioo: inchi 6.42 (19.5:9)
Mfumo endeshi: Android 8.1 (Oreo)
Aina ya Prosesa: Qualcomm SDM845 Snapdragon 845
Ukubwa Prosesa: Octa-core (4×2.8 GHz Kryo 385 Gold & 4×1.7 GHz Kryo 385 Silver)
Ukubwa wa RAM: 8GB
Uhifadhi wa ndani: 256GB
Memori kadi ya nje: Ukubwa mpaka 400GB
Teknolojia mawasiliano: 2G, 3G na 4G
SIM: inatumia Laini mbili
Kamera ya nyuma: Zipo mbili, 16MP na 20MP
Kamera ya mbele: 25MP
Ukubwa Betri: 3730mAh
Aina ya Betri: Li-Ion
Rangi ya simu: Nyekundu na Bluu
Ulinzi: Uwezo wa kutambua sura (Face ID)