Simu ndogo unayoweza ‘Kuizungushazungusha’

0
Sambaza

Kila uchwao katika Dunia ya leo teknolojia imekuwa ikibadilika na kuleta vitu vipya au kuboresha kile kilichopo na kukifanya kiwe bora zaidi.

Simu zipo lukuki ambazo idadi yake ni ngumu kufahamika kwa ujumla lakini ukiwa na simu ambayo unaweza ukaifanya kama mchezo wa kuizungushazungusha si vibaya pia na sasa kwa yeyote yule ambaye anapenda kuchezeachezea simu yake ataifurahia akiwa na simu Chilli Fidget Spinner.

Uzuri wa simu Chilli FIdget Spinner (Simu ndogo ya kuizungushazungusha).

Ni simu yenye uwezo wa kawaida sana (sio simu janja) na hivyo unaweza ukaitumia kama simu mbadala kutokana na uwezo wake wa kutunza chaji kwa muda mrefu sana hivyo kukufanya kutokuwa na hofu wa simu yako kuishiwa na chaji baada ya saa chache.

Sehemu ya kuchomeka chaji ni kama tu simu janja nyingi za Android. Ina diski uhifadhi ukubwa wa 32MB lakini unaweza ukaweka ujazo wa ziada (micro SD card) wa mpaka GB 8.

Kioo chake kina ukubwa wa inchi 1.4 katika rangi sita tofauti tofauti. Haina programu tumishi lakini simu hiyo ina Bluetooth.

Muonekano wa simu ndogo Chill Spinner K188.

Kiitendo cha kuzungushazungusha kitu kama mchezo fulani inasaidia kuondoa mawazo baada ya mihangaiko ya siku nzima hivyo ni kitendo kizuri kitakachosaidia kuondoa fikra mbaya, hasira na kuufanya mwili uchangamke. Tazama picha ya mnato hapo chini.

SOMA PIA:  Zima "Automatic updates" kwenye simu yako

Simu hiyo ndogo imeanza kuuzwa huko nchini India na inauzwa kwa $20 ambazo ni sawa Tsh. 44,980. Kwa sasa upatikanaji wake ni mpaka uagize kupitia masoko mbalimbali kama vile Amazon.

Simu hiyo inatarajiwa kuanza kupatikana kote duniani hivi karibuni. Je, uitainunua simu hii na wewe uifurahie kwa kuizungushazungusha?

Vyanzo: The Verge, Reddit

Facebook Comments

ZINAZOHUSIANA

Sambaza
Share.

About Author

Ni Mhariri Msaidizi na mtaalamu wa mambo yanayohusu kompyuta. Pia ni mmoja wa wafuasi wakubwa katika teknolojia; Dunia ya sasa inaendeshwa kwa teknolojia. Wasiliana nami kupitia |ericmato@teknokona.com|

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com