Simu ya Google yadukuliwa ndani ya dakika moja.

0
Sambaza

Kundi moja la wadukuzi kutoka china limefanikiwa kuidukua simu ya Google Pixel (simu mpya kutoka Google ambayo imejizolea sifa nyingi mitaaani), sio tu kwamba kundi hili lilifanikiwa kuidukua simu hiyo bali lilitumia muda usio zidi dakika 60 kupenya katika kuta za usalama za simu hiyo.

simu ya google

Google pixel

Mapumziko ya mwisho wa wiki ya wiki iliyopita lazima yalikuwa ni ya msisimko kwa kundi la wadukuzi (wenye nianjema) la Qihoo 360 baada ya kufanikiwa kuondoka na kitita cha dola za kimarekani 520,000 pesa taslimu, kundi hili lilijipatia mpunga huo mnene baada ya kufanikiwa kushinda shindano la udukuzi kwa kuzidukua simu na app kadhaa.

SOMA PIA:  Uwezo wa kurudisha kile kilichokuwa kimehifadhiwa kwenye memori ya simu

Qihoo 360 waliwaacha walimwengu midomo wazi baada ya kufanikiwa kudukua simu mpya ya Google ambayo imepata sifa nyingi kutoka kwa mitandao ya teknolojia na uchambuzi ya Google Pixel, lililo washangaza watu zaidi ni kundi hili kutumia sekunde 60 tu.

simu ya google

Picha kutoka mtandaoni.

Tuwaachie wadukuzi somo zima la jinsi ya walivyo fanikiwa kufanya utundu huu lakini jambo la msingi kuelewa ni kwamba Google waliahidi kuziba mwanya (ambao wadukuzi hao kutoka china walitumia) ndani ya masaa ishrini na nne ili kuzuia wadukuzi wengine.

SOMA PIA:  Hivi karibuni utaweza kufuta ujumbe uliokwishatumwa WhatsApp

Mmiliki wa iPhone usiwacheke mapema watu wa android  kwasababu mkwanja walipowa wachina hawa ni pamoja na baada ya kufanikiwa kudukua browser ya Safari ambayo ilikuwa inaendeshwa katika MacOS Sierra na kwa taarifa yako tu hapa iliwachukua sekunde ishirini😂😂😂😂😂.

Facebook Comments
Sambaza
Share.

Comments are closed.

error: Hakimiliki @Teknokona!! Wasiliana nasi kuweza kupata ruhusa ya kutumia mhariri@teknokona.com