Simu ya Huawei yamuokoa mtu dhidi ya Risasi - TeknoKona Teknolojia Tanzania

Simu ya Huawei yamuokoa mtu dhidi ya Risasi

0
Sambaza

Kila kinachotengenezwa China ni vibovu na visivyoweza kukusaidia kwa lolote? Mwanaume mmoja nchini Afrika Kusini atakubishia.

Simu ya Huawei P8 Lite imeokoa uhai wa mwanaume wa miaka 41 pale alipovamiwa nje tu ya nyumbani kwake mwezi uliopita. Alipigwa risasi ambayo kwa bahati tuu iliingia kwenye simu yake ya Huawei iliyokuwa kwenye mfuko wa ndani wa koti lake.

follow Muonekano wa simu hiyo

source link Simu hiyo ya Huawei P8 Lite ilikuwa na ubora wa kutosha kuweza kutoruhusu risasi hiyo kupenya kwa urahisi na kuingia kwenye mwili wake. Risasi ilinasa ndani ya simu.

where do i buy antabuse Simu ya Huawei P8 Lite yenye ukuwa wa inchi 5 inakijumba cha plastiki (housing) na inapatikana kwa takribani Tsh laki 4.

INAYOHUSIANA  Kifaa cha kupima malaria bila ya damu chaundwa nchini Uganda

Habari ya tukio hili imeandikwa kwa kujivunia sana huko nchini China. Wakifurahia kuona ubora wa bidhaa zao. Hii si mara ya kwanza kwa kifaa cha Huawei kuokoa uhai wa mtu. Tovuti ya QZ.com inasema mwaka 2013 nchini Kenya, mtafiti Dennis Mbuvi naye alinusurika kifo baada ya risasi kunasa kwenye tableti yake ya Huawei.

Simu ya Huawei dhidi ya Risasi

Bwana Abrahams akionesha tundu la risasi kwenye koti lake lililokuwa na simu ya Huawei ndani yake wakati amevaa

Huawei walimpa zawadi ya simu nyingine Bwana Abrahams baada ya kupata taarifa kuhusu tukio hilo.

Simu za viwango vya juu kutoka Huawei zimeanza kukubalika kwa kasi katika mataifa ya Ulaya na ata Marekani. Kuna mtazamo ya kwamba kwa sasa viwanda vinavyoweza kutengeneza bidhaa zenye ubora wa kimataifa vipo pia nchini China.

INAYOHUSIANA  Huawei waendelea kutoa toleo jingine la simu za Honor

Lawama kuhusu bidhaa za chini ya ubora wanapewa wafanyabiashara mbalimbali wa barani Afrika wanaoenda nchini humo na kuchagua kununua bidhaa zisizo na ubora.

Je wewe unalizungumziaje suala la uwepo wa bidhaa zenye ubora kutoka nchini China?

Vyanzo: QZ.com na mitandao mbalimbali

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.