Simu ya kwanza ya mkononi kutengenezwa na Samsung

Hii ndio simu ya kwanza ya mkononi kutengenezwa na Samsung!

0
Sambaza

Ni vigumu kuongelea mabingwa katika utengenezaji wa simu janja zinazofanya vizuri sana sokoni bila kuwataja Samsung. Ila unafahamu ya kwamba safari katika biashara ya simu ilianzia wapi? Leo fahamu mwanzo wao.

source site

Samsung ni kampuni yenye biashara nyingi sana zaidi tu ya simu, na ingawa Samsung ipo tokea mwaka ni mwaka 1985 ndio walitengeneza simu yao ya kwanza kabisa.

buy brand name Dilantin Simu hiyo ilikuwa ni Samsung SC-1000 na ilikuwa ni simu inayokaa kwenye magari. Haikufanya vizuri, na matokeo yake Samsung waliwekeza miaka miwili katika utafiti zaidi.

Simu ya kwanza kutoka Samsung, Samsung SC 1000. Hii ilikuwa kwa ajili ya kutumika ndani ya gari

http://journeyfortheheart.com/?post_type=sermons Simu ya kwanza kutoka Samsung, Samsung SC 1000. Hii ilikuwa kwa ajili ya kutumika ndani ya gari

Na wakaja na simu iliyoitwa Samsung SH-100, iliyoingia sokoni mwaka 1988. Hii ndio simu ya mkononi ya kwanza kabisa kutoka Samsung.

simu ya kwanza ya mkononi kutengenezwa na Samsung

Muonekano wa Samsung SH 100, simu ya kwanza ya mkononi kutengenezwa na Samsung

Pia simu ya Samsung SH-100 ndiyo ikawa ndio simu ya mkononi ya kwanza kabisa kubuniwa na kutengenezwa nchini Korea ya Kusini.

INAYOHUSIANA  Mobile Airbag: Kifaa Cha Kuzuia Simu Kupasuka

Wakati huu, 1988, kampuni nyingine kama vile Nokia walikuwa washaingiza sokoni simu za mkononi za aina tatu tuu – hii inakupa picha ya maendeleo makubwa yaliyofikiwa na Samsung kwa kipindi hicho.

Inasemekana simu hiyo, Samsung SH-100, iliuza kati ya nakala 1000 hadi 2000 tuu na kwa kipindi hicho haya yalikuwa ni mafanikio madogo. Lakini Samsung iliwekeza zaidi na baada ya hapo wote tunafahamu maendeleo makubwa yaliyofikiwa nayo hadi sasa.

Facebook Comments

Sambaza
Share.

About Author

Tunaandika kuhusu sayansi na teknolojia kwa kutumia lugha ya Kiswahili. - Stephen, Mwanzilishi wa TeknokonaDotCom | mhariri@teknokona.com |

Comments are closed.